LIGI KUU HISPANIA LA LIGA BBVA MSIMU WA 2016/2017 SUMMARY YA MSIMU MZIMA TOKEA ULIPOANZA AGOSTI 19 ,2016 MPAKA ULIPOISHIA TAREHE 21 MEI,2017

la liga 2017

MSN v bbc.jpgLIGI KUU SOKA HISPANIA LA LIGA BBVA 2016/2017 ” Ni msimu wa 86 tokea ligi kuu ya soka nchini Hispania ilipoanzishwa mwaka 1892″

 • Nchi:  Hispania
 • Bara:  Ulaya
 • Ilianzishwa: Jumapili jioni Julai 3, 1892
 • Mdhamini:  Banco Bilibao Vizcaya Argentaria BBVA
 • Idadi ya Timu:  20
 • Idadi ya timu(Uefa):  4
 • Idadi ya timu (Europa):  Zaidi ya 3+
 • Timu zinazoshuka daraja: 3
 • Ubora:  Mkubwa sana #2 Mashabiki / #1 Kimafaniko
 • Timu bora muda wote:  Barcelona ,Real madrid, sevilla & Athletico madrid
 • Bingwa: Real Madrid(mara ya 33)
 • Bingwa msimu uliopita: FC BARCELONA  (mara 24)
 • Bingwa mara nyingi: Real Madrid (mara 33)

 

BINGWA real mad

 •  Real madrid (Mara ya 33)
Timu zitakazocheza UEFA msimu wa  2017/2018
 • Barcelona
 • Real Madrid
 • Atlético Madrid
 • Sevilla
Timu zinazoshuka Daraja msimu wa 2016/2017
 • Sporting Gijon
 • Osasuna
 • Granada
Mfungaji bora King Leo Messi.jpgLionel Messi
(Magoli 37) Ameingia kwenye rekodi kwa kuwa moja ya mchezaji wa aliyeshinda tuzo ya Pichichi Mara nyingi  (Hii ikiwa mara ya 4)
Timu iliyoshinda mechi nyingi  Real madrid (mechi 29)
VIPIGO VIKUBWA
 • BARCELONA 7-1 Osasuna
 • Atlético Madrid 7–1 Granada
 • BARCELONA 6-0 Alaves
Timu iliyofungwa mechi nyingi Granada (mechi 25)
Ushindi mkubwa mfululizo
 • Barcelona (mechi 6)
 • Real madrid (mechi 6)
Timu iliyoweza kutokufungwa mechi nyingi mfululizo
 • BARCELONA (mechi 20)
Timu iliyofunga magoli mengi
 • BARCELONA
Timu iliyofungwa mechi nyingi mfululizo
 • Granada (mechi 7)
Mechi iliyohudhuriwa na mashabiki wengi Watu zaidi ya elfu 98,486

 • Barcelona vs Real madrid tarehe 3 mwezi wa 12 mwaka 2016 uwanjani Nou camp
Mechi iliyohuduriwa na mashabiki wachache zaidi Watu elfu 3,576

 • Eibar Vs Valencia tarehe 27 Agosti 2016 uwanjani Ipurua Municipal Stadium 
la liga 2017.png

Msimu ulianza kama kawaida timu wababe wa ligi hii yaani FC Barcelona na Real Madrid, bila kusahau Sevilla na Athletico Madrid zikipigiwa upatu wa kuibuka mabingwa wa ligi kuu Hispania msimu wa 2016/2017 .

Hatuna budi wote kukubaliana kuwa Ligi kuu ya Hispania pamoja na ile ya England zimekwisha kwa utata japokuwa si mkubwa sana hususani La liga imetuchukua mpaka mzunguko wa mwisho kumfahamu bingwa. Haikuwa kazi rahisi kwa timu ya Real madrid kushinda ubingwa huku pongezi zikiwa endea washambuliaji hatari kama Ronaldo ,Benzema ,Morata na viungo wazuri kama Isco ambao wamepigania timu hadi kupokonya taji mikononi mwa timu namba moja kwa ubora timu ya FC Barcelona (kwa mujibu wa FIFA) Chini ya Safu ya ushambuliaji hatari zaidi kwenye ulimwengu wa soka hivi sasa MSN.

Timu kama Atletico Madrid na Sevilla zimekuwa na ubora kwa misimu mingi lakini bado hazijawa na uwezo wa kuondoa utawala wa miaba ya soka nchini Hispania yaani Barcelona & Real Madrid.  Kwa hayo na mengine mengi hebu tuende moja kwa moja kutazama timu nne za juu zilizopigiwa upatu wa kushinda ligi kuu hispania msimu wa 2016/2017.

 

#1. REAL MADRID (Alama 93

Related image

 • Nchi: Hispania
 • Mji: Madrid
 • Uwanja: Santiago Berenabeu
 • Ligi: La Liga BBVA
 • Ubora: #3 (FIFA)
 • Utajiri: #1
 • Kocha: Zidane
 • La liga 2016/2017: #1 Bingwa

Usipime !!!!!! Hatuwezi kusema walilipania lakini imani ya wengi ni kwamba ile kiu ya kukosa ubingwa wa La liga kwa misimu mitano mfululizo hatimaye vijana wa madrid wamedhihirisha kuwa wao ni bora kwa kushinda taji la mara ya 33 huku wakizidi kujikita kuwa vinara wa La liga kwa kushinda mataji mengi ya ligi hiyo bora duniani. Ikizingatia na mafanikio timu iliyoyapata msimu huu kwa kuingi hatua ya Fainali katika michuano mikubwa kabisa kuliko yote ya soka kwa ngazi ya klabu UEFA CHAMPIONS LEAGUE.

Haikuwa kazi nyepesi kushinda taji la msimu huu kwani Timu kama fc Barcelona na Athletico De Madrid zilikuwa kwenye ubora wao mkubwa sana kiasi cha kuaminisha safu ya ushambuliaji ya Real madrid ikiongozwa na mshambuliaji hatari na  mchezaji bora wa dunia mara 4 Cristiano Ronaldo imechangia kwa kiasi kikubwa sana kupeleka ubingwa Santiago Berenabeu kwa mara ya 33 huku akiifungia timu yake magoli 25.

 

#2. FC BARCELONA (Pointi 90)

fc Barca squad.jpg

 • Nchi: Hispania
 • Mji: Barcelona
 • Uwanja: Camp Nou
 • Ligi: La Liga BBVA
 • Kocha: Luis Enerique
 • La Liga 2016/2017: #2 (Runner up)
 • Ubora: #1 (FIFA)
 • Utajiri: #2

Mwanzo hawakutegemea kushindwa kutetea ubingwa wao walioshinda kwa mara ya pili mfululizo msimu wa 2015/2016 chini ya kocha Luis Enerique ambaye hatutokuwa naye msimu ujao kama kocha wa Fc Barcelona.

Kiukweli na sio siri Klabu ya Barcelona ni tishio sana ikiongozwa na safu ya Ushambuliaji yenye Rate na kiwango bora sana kuliko safu ya timu yoyote ile kwa hivi sasa nazungumzia MSN (Messi, Suarez na Neymar) . Ubora wa hawa jamaa haufichiki ni washambuliaji hatari sana ambao kila mwaka wote watatu huingia kwenye kikosi bora cha mwaka cha FIFA ! zaidi ya hilo mpaka ligi kuu ya hispania msimu wa 2016/2017 uliomalizika wafungaji bora 10  MSN imo huku wafungaji bora wajuu kabisa akiwa mchezaji aliyezaliwa kufunga maarufu kwa jina GOAL MACHINE yaani Luis Suarez (magoli 29 bila penati) na mchezaji bora zaidi duniani  Lionel Messi (aliyeibuka mfungaji bora kwa idadi ya magoli 37). Kwa vigezo hivyo na vingine Barcelona ilipigiwa upatu zaidi yumkini kuliko timu zingine. Lakini kichapo dhidi ya malaga kilifanya wapinzani wao wakubwa Real Madrid kusogeza kombe sembuleni na hatimaye kuwa mabingwa. Ubora wa Messi, Suarez na Neymar haukutosha kushinda ligi kuu la liga 2016/2017 licha ya kumaliza kwa heshima kubwa mbele ya Eibar kwa kichapo cha bao 4 -2 uwanjani Nou Camp.

 

 

#3. ATLETICO DE MADRID (pointi 78)

Athletico madrid squad.jpg

 • Nchi: Hispania
 • Mji: Madrid
 • UwanjaVicente Calderón Stadium
 • Ligi: La Liga BBVA
 • Kocha: Diego Simione
 • Ubora: #7
 • Utajiri: #11
 • La liga 2016/2017: #3

Chini ya kocha machachari mwenye vituko na bwembwe kibao Diego Simione . mwanzo mzuri ukichagigzwa na historia ya kunyakua taji la La Liga msimu wa 2012/2013 na mwenendo mzuri kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya kulifanya wengi waamini kama sio tu kuleta ushindani mkubwa au hata kutwaa ndoo ya La liga msimu wa 2016/2017 kabla ya ndoto zao kufifizwa na kuteteleka na matokeo yasiyo mazuri katikati na mwishoni mwa msimu .

Licha ya hilo Atletico De Madrid isiyo na matumaini ya ubingwa wa aina yoyote ni timu nzuri iliyosheheni wachezaji bora na hatari kama vile Fernandon Torres na Antonio Gerzmann ambao wamepegania timu hadi kumaliza kwenye nafasi za juu za La Liga huku wakijihakikishia kushiriki kwenye Ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2017/2017 ikiungana na Real madrid ambayo msimu huu mambo yanaonekana kuiendea vizuri sambamba na Wazamisha nyambizi kwa vipigo vikubwa Fc Barcelona bila kusahau Sevilla.

 

HII NI SUMMARY FUPI AMBAYO TUMEJARIBU KUONA UWEZO NA MATUMAINI YA TIMU ZILIZOPIGIWA UPATU WA KUNYAKUA TAJI LA LA LIGA 2016/2017. TUMESHUHUDIA REAL MADRID IKIWA BINGWA WA LA LIGA 2016/2017 . SWALI NI JE WATAWEZA KULITETEA MSIMU UJAO ?!  WAZAMISHA NYAMBIZI ( BARCELONA) WTAKUBALI KULIKOSA HUKU WAKIWA NA KIKOSI IMARA NA GHARI ZAIDI ?! VIPI TIMU ZINGINE ZITAKUBALI KUWA WASINDIKIZAJI ????!!!!!!! MMMMMMhhh MI SIJUI TUPE MAONI YAKO HUKU TUKIENDELEA KUSUBIRI MSIMU UJAO WA LA LIGA BBVA 2017/2018.

O1 SPORTS ni jarida la watu na linahitaji maoni yako kwenye hili huku likikukumbusha wewe mpenzi wa soka usikose kufuatilia matukio makubwa kabisa yatakayojiri hivi punde kwenye

 1. KOMBE LA MABARA URUSI 2017
 2. MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA 2018 URUSI 

U            S           I         K           O                S                    E

Tunajua sana uwepo wako ndio maana tunahakikisha tunakuletea vitu vizuri siku zote. Tafadhali Tutembelee leo kwenye  www.Nijuzepedia.com/01 sports

 • Vilevile unaweza kusoma Summary nzima ya Ligi kuu England msimu wa 2016/2017 ambapo CHELSEA F.C imeshatangaza ubingwa kwa msimu wa 2016/2017 Bonyeza HAPA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sponsored by GOAL EXPRESS

 

© 2017 Powered by 01 SPORTS

Advertisements

Leave Comment / Toa Maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s