LIGI KUU ENGLAND EPL MSIMU WA 2016/2017 SUMMARY YA LIGI NZIMA TANGU ILIPOANZA RASMI AGOSTI 6 2016 MPAKA ILIVYOISHA MEI 21 2017

Chelsea-home-kit-2015-16-02.jpg

OABLIGI KUU  SOKA ENGLAND 2016/2017 ” Ni ligi kuu soka England msimu wa 25 tangu ilipoanzishwa rasmi mwaka 1992 lakini ilikuwepo tokea mwaka 1888 ikijulikana kama ligi ilijumuisha timu za soka za england huku ikiwa ndio Ligi kongwe zaidi kuliko zote duniani”

 • Nchi:   Uingereza (England&wales)
 • Bara: Ulaya
 • Mdhamini:  Hakuna
 • Ilianzishwa: mwaka 1888
 • Ilianzishwa rasmi: mwaka1995
 • Idadi ya timu: 20
 • Idadi ya timu (UEFA): 4
 • Timu zinazoshuka daraja: 3
 • Ubora: Mkubwa sana 1# Mashabiki, 2#Kimafaniko
 • Timu bora muda wote: Zaidi ya 6+ (Manchester United, Chelsea, Liverpool, Arsenal, Manchester city, Tottenharm hotspurs, na nyingine nyingi)
 • Bingwa msimu huu: CHELSEA F.C ( Mara 5)
 • Bingwa mara nyingi: Manchester United (mara 13)
BINGWA Chelsea mabingwa lCHELSEA F.C

“Mara ya 5”

Timu zinazoshuka daraja
 • Hull City
 • Middlesbrough
 • Sunderland
Timu zitakazo shiriki UEFA  2017/2018
 • Chelsea
 • Tottenham Hotspur
 • Liverpool
 • Man city au Arsenal 
 • Man United kama ikishinda EUROPA
Timu zitakazo shiriki Europa 2017/2018
 • Everton
 • Arsenal au Man United(hatua ya makundi)
Idadi ya mechi zilizochezwa 367
Mfungaji bora harry kHarry Kane
(Magoli 29 )
Vichapo vikubwa
 • AFC Bournemouth 6–1 Hull City
 • Chelsea 5–0 Everton
 • Liverpool 6–1 Watford
 • Tottenham Hotspur 5–0 Swansea City
 • Manchester City 5–0 Crystal Palace
 • Stoke City 0–4 Tottenham Hotspur
 • West Bromwich Albion 0–4 Manchester City
 • West Ham United 1–5 Arsenal
 • Swansea City 0–4 Arsenal
 • West Ham United 0–4 Manchester City
 • Crystal Palace 0–4 Sunderland
 • Sunderland 0–4 Southampton
 • West Ham United 0–4 Liverpool
Timu iliyoshinda Mechi nyingi CHELSEA F.C (Mechi 13)
Timu iliyofungwa mechi chache Tottenharm (Mechi 4)
Timu iliyofungwa mechi nyingi Sunderland (mechi 24)
Mechi iliyoshuhudiwa na mashabiki wengi Uwanjani
 • Mashabiki Elfu 75,397             Manchester United VS  West Bromwich Albion Tarehe 1 April 2017 Uwanjani OLD TRAFORD
Mechi iliyoshudiwa na watu wachache zaidi uwanjani
 • Mashabiki elfu 10,890

AFC Bournemouth Vs Middlesbrough
Tarehe 22 April 2017 Uwanjani Dean Court

UBORA WA LIGI FIVE STARS.jpg# MZURI
lolling emoji

 • Hahahahahaha!!! Ligi ya ajabu sana hii
 • CHELSEA FCimeshinda msimu wa 2016/2017 LEICESTER CITY alikuwa bingwa mtetezi amemaliza ligi akiwa nafasi ya  11
 • UNAKUMBUKA LAKINI ??????!!!! LEICESTER CITY Ilishinda taji la epl 2015/2016 ikipola kutoka kwa CHELSEA na kuifanya The Blues kushika nafasi ya 10 .

Ligi ilianza kwa kishindo huku timu kadhaa zikipewa upatu wa kuchukua ligi zikiwemo Manchester United, Manchester city, Liverpool ,Tottenharm Hotspurs, Arsenal na Chelsea ambayo ndio timu iliyofanikiwa kushinda taji la Epl msimu wa 2016/2017.

Timu hizo zilizopigiwa upatu zilikuwa na vigezo kadhaa vilivyopelekewa kupewa nafasi kubwa ya kushinda taji la ligi ambazo ni zifuatazo:

cheleaCHELSEA F.C                                                                                    Ujio wa kocha aliyekuwa wa Timu ya taifa ya Italia Antonio Konte na usajiri wa kiungo bora sana Ngolo Kante na ubora wa safu ya ulinzi pamoja na ya kiungo bila kusahau ya ushamburiaji huku kila mtu akiwa shahidi uwezo na kiwango cha daraja la kwanza cha Kiungo mshambuliaji Eden Harzard ambaye licha tu yakuwa moja ya wafungaji bora kwenye msimu huu wa 2016/2017 tokea mwanzoni mwa msimu alichagiza mbio za ubingwa kwa kiwango cha hali ya juu sana. Ubingwa wa chelsea kwa maoni ya wengi umechangiwa na Safu ya ulinzi ,viungo wazuri na safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Diego Costa ambaye mpaka ligi inaisha yuko kwenye orodha ya juu kabisa ya wafungaji akiwa na magoli zaidi ya 20.

 • t full

TOTTENHARM HOTSPURS                                                       Kama ilivyo kwa timu nyingine zilizopigiwa upatu licha ya kutolewa mapema kabisa kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya UEFA CHAMPIONS LEAGUE timu hii iliendelea kupigiwa upatu na wadau pamoja na mashabiki wa soka kote duniani kuwa itafanya vizuri kwenye ligi kuu england ikizingatiwa kuwa ilikuwa ikichagiza ubingwa dhidi ya Leicester City  kwenye msimu wa 2015/2016 bila kusahau washambuliaji bora sana Harry Kane na Delle Ali ambao kiukweli wamejitahidi sana kuhakikisha timu yao inafikia mahali pazuri licha ya kukosa ubingwa lakini wakijihakikishia nafasi ya kushiriki Ligi ya klabu bingwa barani ulaya UEFA msimu wa 2017/2018.

 • liverpoll

LIVERPOOL F.C                                                                            Ubora wa akina Coutinho , Mane ,Lalana na wengine wengi haukutiliwa shaka kabisa mwanzoni mwa msimu wa EPL 2016/2017  kwa kuwa mashabiki wengi wa soka walijua wazi kuwa timu ya Liverpool ingifanya vizuri sana kwenye ligi huku jambo hili likichagizwa na vichapo vikubwa na mwanzo mzuri wa wa msimu , Ingawa jambo hili liliingia doa baada ya majeruhi mwishoni mwa mwaka 2016 jambo ambalo lilipunguza kasi ya timu kuelekea ubingwa wa epl 2016/2017. licha ya hayo Liverpool mpaka mwisho wa msimu tayari ilikuwa imejihakikishia nafasi ya kucheza UEFA msimu wa 2017/2018.

 • Manchester_City_2016

MANCHESTER CITY                                                                       Ubora wa kikosi na ujio wa kocha mwenye mafaniko sana kwenye soka Pepe Guadiola akitokea Bayern Munich ambako pia alikuwa na mafaniko lukuki bila kusahau yale aliyoyapata akiwa na “Wazamisha nyambizi” Timu hatari na bora zaidi duniani kwa mujibu wa FIFA klabu ya F.C BARCELONA .  Jambo hili liliwaaminisha wengi kuwa kocha huyu ataleta mafanikio makubwa na hata kuchukua taji la epl huku imani ya mashabiki ikiongezeka kutokana na vipigo vikubwa vilivyokuwa vikitolewa na timu hiyo yenye maskani yake jijini Manchester. Kukosa ubingwa kwa Man city ni jambo ambalo halikupewa nafasi lakini kutokana na ushundani uliopo miongoni mwa timu za ligi hiyo ni jambo lisiloshangaza maana CHELSEA  mpaka inashinda taji msimu wa nyuma ilishika nafasi ya 10 , huku Leicester city  aliyekuwa bingwa mtetezi msimu wa 2015/2016 akishika nafasi ya 11 msimu ambao CHELSEA  amekuwa bingwa 2016/2017. Hahaha ! Hii ni Hatari. Licha ya hayo Man city iomedhihilisha ni miongoni mwa timu bora kabisa za England baada yakumaliza nafasi za juu za ligi kuu ya epl 2016/2107.

 • arsenal-logo

Si jambo geni kwa shabiki yoyote wa soka kusikia Arsenal kupigiwa upatu wa kushinda kwa kila mwanzo wa msimu kila ligi ya epl inapoanza. Kama ilivyo kawaida mambo hayakuwa tofauti mwanzoni mwa msimu wa msimu wa epl 2016/2017 Arsenal ilipigiwa upatu wa kushinda ligi kuub england japo mwisho wa siku hali imekuwa tofauti na kuwa msimu ambao wengi wanadai kuwa mbaya zaidi toka arsenal iliposhinda Taji la ligi kuu Epl kwa mara ya mwisho mwaka 2003 . Ambapo imeshuhudiwa Arsenal kwa mara ya kwanza tokea  2003 kumaliza chini ya nafasi nne za juu za epl. Arsenal ambayo kiukweli haiwaridhishi mashabiki wake kwa mwenendo mbaya tofauti na jina kubwa la timu huku kocha Arsene wenger akiendelea kuwa kocha wa klabu hiyo ya London yenye rekodi ya pekee epl ya kushinda taji bila kufungwa Msimu wa 2003 licha ya lawama na kelele za kumtaka kuacha kunoa timu hiyo kutoka kwa baadhi ya mashabiki na wadau wa klabu hiyo.

 • man uMANCHESTER UNITED                                                         Kwa upande wa Manchester United Kutokana na Usajiri  uliovunja rekodi ya uhamisho kidunia kwa pauni milioni 100 wa Paul Pogba na Zaltan Ibrahmovich chini ya kocha mwenye mafanikio makubwa Jose mourincho Manchester United Ilitabiriwa na kupewa upatu wa kuchukua taji huku jambo hilo likichagizwa na mwanzo mzuri kwenye ligi ingawa baada ya matokeo mabovu yaliyokuwa tofauti na kikosi cha timu hii yenye mataji mengi ya Epl hali hii imepelekea kumaliza chini ya nafasi nne za juu za ligi kuu epl huku suala hili likiwa na athari kwa ligi kubwa na maarufu zaidi ya soka ulimwenguni  Ligi kuu ya soka England  kwa kukosa timu nyingi zenye mafanikio ya juu kabisa Huku CHELSEA na LIVERPOOL pekee ndizo timu zinazoonekana kuwa zenye ushindani mkubwa Kwenye ligi za kimataifa hasa UEFA CHAMPIONS LEAGUE  tofauti na Man city pamoja na Tottenharm . Lakini ni jambo la kusubiri ikiwa Man united ikishinda mechi ya Fainali ya EUROPA dhidi ya Ajax basi itapata nafasi ya moja kwa moja ya kushiriki  UEFA msimu wa 2017/2018 na kuchagiza mbio za kukata kiu ya Ubingwa wa ulaya kwa timu za EPL .

 

Shukrani kwa kusoma na unakaribishwa kutoa maoni bila kusahau vilevile unaweza soma SUMMARY YA LA LIGA MSIMU WA 2016/2017 kwa kubofya HAPA 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sponsored by GOAL EXPRESS 

© 2017 Powered by 01 SPORTS

Advertisements

Comments

6 comments on “LIGI KUU ENGLAND EPL MSIMU WA 2016/2017 SUMMARY YA LIGI NZIMA TANGU ILIPOANZA RASMI AGOSTI 6 2016 MPAKA ILIVYOISHA MEI 21 2017”
 1. forex says:

  Some truly nice and useful info on this site, likewise I believe the style and design has excellent features.

  Like

  1. THANK YA SO MUCH FOREX ! We really appreciatin’ what ya saying we woulda like to hear many other comments from you.. Keep ballin’ with us please !

   Like

  2. THANK YA SO MUCH FOREX, Hopeful you gonna still be on our side thank you so much

   Like

 2. xxx says:

  Thɑnks for sharing your thoughts on bad. Regards

  Like

 3. read review says:

  certainly, the environmental news theses days are not so good but there are other good news too like opening of new forest reserves“

  Like

 4. buy condoms says:

  Woah! I’m really digging the template/theme of this site.
  It’s simple, yet effective. A lot of times it’s very difficult
  to get that “perfect balance” between user friendliness and visual appeal.

  I must say that you’ve done a awesome job with this.
  Also, the blog loads super quick for me on Opera. Outstanding Blog!

  Is it OK to post on Google+? Keep up the excellent
  work!

  Like

Leave Comment / Toa Maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s