CRDB bank Tanzania &  East African banks…. Benki ya CRDB  Tanzania  

 

MAKAO MAKUU: Dar es salaam
NCHI: Tanzania
ILIANZISHWA: Mwaka 1996
ENEO LA HUDUMA:

NCHI 2

  • Tanzania
  • Burundi
MAPATO KWA MWAKA: Zaidi ya USD millioni 50 +
UTAJIRI [makadirio] : Zaidi ya Tsh trillioni 4
HISA:

Dar es salaam stock exchange DSE

  • Iliingizwa rasmi Juni 2009
MTANDAO WA UENEAJI:
  • ATM Machines 430 +
  • Point of sales Terminals 770+
  • Mawakala Fahari huduma 1765+
MATAWI:  Zaidi ya 195+
IDADI YA WAFANYAKAZI: Zaidi ya 2,150+
NAFASI :

#1 Tanzania

KAULI MBIU:

The Bank that listen [Benki inayomsikiliza mteja]

Tovuti / Website www.Crdbbank.com

Hii ni benki inayoongoza nchini Tanzania katika vigezo mbalimbali ikiwemo suala la utoaji wa mikopo ,, huduma za kisasa za  kuweka na kutoa pesa  pamoja na umiliki wa mali nyingi kuliko benki zingine nchini Tanzania. Ilianzishwa na serikali chini ya sheria ya makampuni kifungu cha 212 kifungu kidogo cha 12 zaidi ya miaka 20 iliyopita jijini Dar es salaam kama taasisi ya fedha ya maendeleo iliyokuwa na lengo la maendeleo  vijijini yaani Cooperative Rular Development mwaka 1996, wakati huo serikali ikiwa inaumiliki wa asilimia 100% juu ya hisa za benki hii kabla ya kubinafisishwa.

Kwa sasa ni wazi kwamba inatajwa na watu wengi nchini Tanzania kama benki yenye mafanikio zaidi Kiteknolojia , kiueneaji, huduma za haraka na nzuri , mauzo mazuri ya Hisa pamoja na mengine mengi. 

Katika kujiimarisha zaidi kibiashara Crdb ilijiunga rasmi na soko la hisa la Dar es salaam DSE Juni 17 mwaka 2009. Na imezidi kuonyesha nia ya kupanua huduma zake ndani na nje ya ukanda wa Afrika Mashariki. Huku ikishuhudiwa ufunguzi wa huduma na matawi ya benki hii nchini Burundi mwaka 2012.

Hii ndio benki ya CRDB tembelea matawi yao kwa mahitaji yako ya kibenki ukiwa Tanzania na Burundi.

 

FOR TRANSLATION IN YOUR FAVORITE  LANGUAGE  

  • View full site if ya using cellphone & tablet
  • Click on select language For personal computer PC
Advertisements