TOP 6 VING’AMUZI BORA NA MAARUFU VYENYE  WATEJA WENGI NA MATUMIZI MAKUBWA  YA KILA SIKU NCHINI TANZANIA 

Baada ya kuhamia rasmi kwenye mfumo wa kisasa wa kurushia matangazo ya satelite (digital)  nchi ya Tanzania Imeshuhudia huduma za ving’amuzi kwa ajiri ya matangazo ya runinga kwa namna ya kisasa kabisa.
Ubora na umaarufu wa king’amuzi  husika hutegemea

 • Ubora wa kurusha matangazo.
 • Ubora wa vifurushi.
 • Uwezo wa king’amuzi kutoa huduma bila matatizo yoyote ya kiufundi ya mara kwa mara.
 • Uzuri wa picha na sauti  wa king’amuzi  husika.
 • Wingi wa channels.
 • Eneo la utoaji wa huduma wa king’amuzi husika.
 • Ubunifu pamoja na channels zenye kutazamwa sana  N. K

Kwa vigezo hivyo na vingine  hivi ndio ving’amuzi  bora na maarufu zaidi vyenye wateja wengi zaidi nchini Tanzania.

 

#6.

The CONTINENTAL DECODER

MAKAO MAKUU:   Ilemela, Mwanza

NCHI:  Tanzania

KILIANZISHWA  Mwaka 2013

MMILIKI:  Sahara media group

IDADI YA CHANNELS:   50+

IDADI YA VIFURUSHI:   4+

ENEO LA HUDUMA:   Nchi moja [ Tanzania]

TEKNOLOJIA:

 •  D.T.T  / D.D.T.V
 •  HD
 • I.P.T.V
 • Digital cable

UBORA:

 • Picha
 • Sauti
 • Uwezo wa kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa:

KAULI MBIU:  “The quality to talk about”

UMAARUFU [Tanzania]: #2

 

 

Uzalendo pamoja na uchu wa kuhakikisha watanzania wanaondokana na mfumo wa kianalogia king’amuzi hiki kiko mstari wa mbele kabisa kwenye suala hili. Continental ni king’amuzi chenye idadi ya watumiaji wengi nchini Tanzania huku kampuni ikiwa na mipango ya kusambaza huduma katika nchi mbalimbali. Na inasadikika kuwa king’amuzi hiki ndicho kinachoongoza kwenye teknolojia ya kisasa kabisa ya Digital Terrestial Television yaani D.D.T.  

Teknolojia hii ni mapindunzi makubwa sana katika ulinwengu wa television na digital kwa ujumla huku  ikiwa imeboresha sana mwonekano na sauti kwenye runinga. Continental decorder inajitahidi sana licha ya matatizo ya kiufundi, kitendo cha  huduma kwa wateja pamoja na kutosambaa nchi nyingi kama watumaji wake wanavyodai.

Kampuni mmiliki wa king’amuzi hiki Sahara media group  ni kampuni makini sana ambayo imani ya wengi kutokana na mafanikio ya kampuni hii inapelekea kuamini tatizo lolote litakalojitokeza linatatuliwa kutokana na maboresho yanayoendelea kila siku.

Licha ya hayo Continental decorder ni king’amuzi bora na maarufu sana chenye matumizi sehemu nyingi nchini Tanzania.

 

 

 

#5.

STARTIMES

MAKAO MAKUU: Beijing

NCHI: China

KILIANZISHWA:  Mwaka 1988

MMILIKI: Startimes digital  group

IDADI YA CHANNELS: 150 +

IDADI YA VIFURUSHI:   6+

ENEO LA HUDUMA [ Afrika ]Nchi 7 

 • Tanzania
 • Kenya
 • Uganda
 • Rwanda
 • Afrika ya kati
 • Nigeria
 • Afrika kusini

TEKNOLOJIA

 • D.D.T.V
 • H.D
 • D.T.H
 • Digital cable & Non cable Digital Tv

UBORA:

 • Picha
 • Sauti
 • Uwezo wa kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa:

KAULI MBIU:  ” Enjoy Digital Life

 

 

Ni ukweli usiopingika hata kidogo kuhusu ubora wa king’amuzi hiki ambacho ni moja ya ving’amzi vya awali kabisa kutoa huduma za kidigital nchini Tanzania. Kampuni inyomiliki king’amuzi hiki ni wazi kwamba ni kampuni kubwa duniani kutoka nchini Uchina. Teknolojia za hali ya juu kabisa zinazounda bidhaa hii hukifanya kwa bora sana .

Startimes ni maarufu imeenea sana Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika huku kampuni ikiwa imedhamiria khakikisha inawafikia watumiaji wengi katika sehemu mbalimbali. King’amuzi hiki licha ya kusimamiwa na kampuni kubwa lakini bado haijakidhi mahitaji ya baadhi ya watanzania hasa wanaopenda kuona ubunifu mpya hususani juu ya  ongezeko la channels kwa gharama wanayoweza kuimudu.

Licha ya hili Startimes ikumbukwe kuwa kwa upande wa burudani hasa kwa wapenda soka ndicho king’amzi chenye mksanyiko wa vifurushi vinavyomuwezesha mteja kufurahia  LIGI ZA SOKA BORA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI. kwa gharama ndogo ukilinganisha na DSTV. 

Kwa upande wa kiufundi king’amuzi hiki hakujawa na malalamiko mengi japokuwa matatizo ya kifundi hayana budi kutokea kutokana na sababu mbalimbali.  King’amzi hiki kinazidi kutoa huduma nzuri kabisa nchini Tanzania huku kikijivunia kuwa moja ya ving’amuzi vyenye vitengo bora vya huduma kwa wateja nchini Tanzania.

 

 

 

 

#4.

TING HD

 

MAKAO MAKUU Mbezi , Dar es salaam

NCHI:   Tanzania

KILIANZISHWA:  Mwaka 2009

MMILIKI:  Tanzania intergrated network group 

IDADI YA CHANNELS:  100+

IDADI YA VIFURUSHI: 3+

ENEO LA HUDUMA:  Tanzania

TEKNOLOJIA:

 • D.T.T
 • High Definition 
 • I.P.T.V
 • D.T.H
 • Digital cable

 

UBORA:

 • Picha
 • Sauti
 • Uwezo wa kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa

 

KAULI MBIU: ” BORA KULIKO

UMAARUFU [ Tanzania ]:  #5

 

King’amuzi rahisi chenye gharama nafuu sana ,wateja wengi ubunifu wa hali ya juu ,uzoefu na huduma nzuri kwa mteja , bila shaka unakuwa hujakosea kutaja Ting HD  King’amuzi bora sana nchi Tanzania huku kikitoa huduma nzuri kwa gharama ndogo kabisa kwa kila mwananchi . Ting ni king’amuzi ni moja ya ving’amuzi viwili vya  awali kabisa kutoa huduma zake nchini Tanzania. Kampuni mmiliki wa king’amuzi hiki inao uzoefu wa kutosha kuhusu utoaji wa huduma za kidigitali  huku king’amuzi chake kikisifiwa kwa kutokuwa na matatizo mengi ya kiufundi.

Ting licha ya mafanikio haya bado haijawafikia wateja wa ving’amuzi kwenye nchi zingine lakini suala hili ni la kimikakati.

Ubora wa picha na sauti pamoja na ongezeko la channels kwa gharama ndogo hufanya king’amuzi hiki kiwe bora na maarufu nchini Tanzania.

 

 

#3.

ZUKU TV

 

MAKAO MAKUU:  Mombasa road, Nairobi

NCHI:  Kenya

KILIANZISHWA:  Mwaka 2011

MMILIKI:  Wananchi group

IDADI YA CHANNELS:   100+

IDADI YA VIFURUSHI:  4+

ENEO LA HUDUMA: Nchi 5

 • Kenya
 • Tanzania
 • Uganda
 • Zambia
 • Malawi

TEKNOLOJIA:

 • D.T.H 
 • H.D
 • S.D
 • D.D.T.V

 

UBORA:

 • Picha
 • Sauti
 • Uwezo wa kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa

 

 

UMAARUFU [ Tanzania ]: #4

 

Mali ya Wananchi group   kampuni yenye mafanikio sana ukanda wa Afrika mashariki kwenye upande wa kutoa burudani kwa familia nyumbani.     king’amuzi cha Zuku Tv  kinao ubora wa kujitosheleza sana kiasi cha kuaminiwa na kutumika na wananchi wa Afrika Mashariki na baadhi ya nchi jirani.

Hamu na umakini wa kampuni unafanya king’amuzi hiki kupata mafanikio makubwa kila kukicha huku wamiliki wakiwa na mipango ya kupanua huduma zao na kuwafikia watu wengi zaidi wenye mahitaji ya kidigital.

Matatizo ya kiufundi haya yapo kwa kila king’amuzi ingawa kwa upande wa Zuku yapo lakini ni ya kawaida ambayo hayana malalamiko sana kutoka kwa wateja huku suala hili likichangiwa sana na umakini wa kitendo cha huduma kwa wateja.

Zuku Tv  ni moja ya king’amuzi bora Afrika mashariki na Tanzania.

 

 

 

#2.

DSTV

 

MAKAO MAKUU:   Randburg, Johhanesburg

NCHI:   Afrika kusini

KILIANZISHWA:  Mwaka 1995

MMILIKI:  Multichoice

IDADI YA CHANNELS:  300+

IDADI YA VIFURUSHI:   10+

ENEO LA HUDUMA: Nchi 9

 • Afrika kusini
 • Tanzania
 • Kenya
 • Nigeria
 • Angola
 • Uganda
 • Zimbambwe
 • Mauritius
 • Ghana

TEKNOLOJIA:

 • H.D.M.I
 • High Definition 1080P
 • D.T.T/ D.D.T.V
 • DIGITAL CABLE 
 • D.T.H

UBORA:

 • Picha
 • Sauti
 • Uwezo wa kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa

KAULI MBIU: “ Feel every moment

UMAARUFU [ Tanzania]: #2

 

Unapotaja ving’amuzi bora Tanzania na barani Afrika kwa ujumla kamwe huwezi kusahau kutaja jina la Digital Satelite Television maarufu sana kwa jina la DSTV. Hiki ndio king’amuzi bora na maarufu zaidi barani Afrika kuliko king’amuzi chochote kile.

Ubora wa hali ya juu sana unaochangiwa na uzoefu wa muda mrefu , umakini , ubunifu bila ya kusahau huduma nzuri sana kwa wateja zilizo karibu, hakika vitu hivi hufanya king’amuzi hiki kuwa bora sana.

Kwa ukweli huu unaweza kujiuliza ” Ni kwa nini king’amuzi hiki ni cha #2 kwenye orodha hii ???!!! ” sababu ni >>>>>>>>>>>>>

Kiukweli gharama za king’amuzi hiki ni ghali ukilinganisha na matumizi pamoja na hali ya uchumi  ya wateja wa ving’amuzi nchini Tanzania ambao wengi wao hawana uwezo wa kumudu gharama za vifurushi vya king’amuzi hiki. Mfano Kifurushi cha gharama ndogo cha king’amuzi hiki kina gharama ya Tsh 23,000/=  gharama ambayo kwenye ving’amuzi vingine inaweza kumuwezesha mtu kununua vifurushi vya hadhi ya kati yaani Premium Packages.

Lakini hupaswi kasahau kuhusu ” kizuri kina gharama” .. Dstv ni king’amuzi kinachoongoza kwa kutoa burudani barani Afrika mfano mzuri wa burudani zinazotolewa na king’amuzi hiki ni Matangazo mbalimbali ya michezo . King’amuzi hiki ndio nyumbani kwa michezo mingi sana ikiwemo Mchezo unaopendwa zaidi duniani mchezo wa Soka huku king’amuzi kikirusha kila mechi ya LIGI ZA SOKA BORA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI. na burudani nyingine nyingi sana ikiwemo Mziki, filamu na kadhalika. Ikumbukwe pia kuwa mwaka 2016  king’amuzi hiki kilichanguliwa kuwa mrusha matangazo rasmi wa michezo ya Olyimpiki jijini Rio de Janeiro.

Ni ukweli ulio wazi kuwa Dstv ni king’amuzi maarufu chenye matumizi kila siku na  bora sana nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla

 

 

 

#1.

AZAM TV

 

MAKAO MAKUU:   Tazara, Dar es salaam

NCHI:  Tanzania

KILIANZISHWA:  Mwaka 2013

MMILIKI:  Bakhresa group of companies

IDADI YA CHANNELS: 100+

IDADI YA VIFURUSHI: 4

ENEO LA HUDUMA:  Nchi 5

 • Tanzania
 • Kenya
 • Uganda
 • Rwanda
 • Malawi

TEKNOLOJIA:

 • High Definition Multimedia Interface
 • HD 1080P
 • Digital Terrestial Television D.T.T
 • Digital cable

UBORA:

 • Picha
 • Sauti
 • Uwezo wa kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa

 

KAULI MBIU: “ Burudani kwa wote

UMAARUFU [ Tanzania ]: #1

 

Burudani kwa wote ” au kwa kiingereza ” Entertainment for everybody ”  Huu ndio msemo maarufu sana  ambao pindi unapotamkwa moja kwa moja mtumiaji wa digital Tv anaelewa ni king’amuzi gani kinakuwa kikizungumziwa.  Sio siri hata kidogo bila mizengwe king’amuzi cha  Azam Tv ni bora sana na asilimia kubwa ya watu wanajua hili.

Kikiwa kinaungwa mkono na teknolojia ya hali ya juu yenye kupelekea mwonekano ang’avu yaani HD wa channels zake . Mbali na hayo king’amuzi hiki kinaongozwa na ubunifu wa pekee na wa kisasa wenye kukidhi mahitaji ya wateja wake kwa gharama za kawaida.

Kikiwa na channels za kutoa habari , vipindi vya watoto , elimu na sayansi, dini pamoja bila kusahau burudani hapo king’amuzi hiki kimejidhihirishia ubora wake kwa kuwa na channels za burudani zinazopendwa sana, Mfano channel ya Sinema zetu  ambayo inaonyesha filamu za kiTanzania kwa asilimia 100% na Azam sports HD ambayo inahakikisha mteja wa king’amuzi hiki hapitwi na mechi yoyote ya Ligi bora kabisa duniani LA LIGA.

Licha ya hayo kudhihirisha utayari wa suala la burudani kwa wote king’amuzi hiki kimedhamini ligi za soka Afrika Mashariki huku channels za  Azam  One na Azam Two.

King’amuzi hiki kinazidi kupata umaarufu na wateja Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla huku kwa wakazi wa Tanzania wakiwa mashahidi kuwa hakuna king’amuzi chenye wateja wengi na kilichosambaa kama hiki.

King’amuzi hiki ni bora sana Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla huku channels Mama za king’amuzi hiki zikiendeshea matangazo yake kutoka kwenye moja ya studio nzuri na kubwa kabisa barani Afrika.

 

 

 

 

 

#Hivyo ndio ving’amuzi maarufu vyenye matumizi makubwa kila siku na bora zaidi nchini Tanzania

#ORODHA KWA NAMBA

 1. Azam Tv
 2. Dstv
 3. Zuku Tv
 4. Ting HD
 5. Startimes
 6. Continental decoder 

 

 

 

 

 

ZINGATIA:

Idadi ya vifurushi pamoja na channels ,Teknolojia , eneo la huduma pamoja na ubora wa king’amuzi husika ni vitu vinavyobadilika badilika hivyo fuatilia  updates ya post bila kusahau kutoa maoni kuhusu suala lolote kuhusu orodha hii ya ving’amuzi nchini Tanzania vilivyo na matumizi, maarufu na bora zaidi na zingine.

Kwa sababu  >>>>>>>>>>

 

 

 

Wewe ni sehemu ya WWW.NIJUZEPEDIA.COM Toa maoni na share na wenzako

 

 

 

Comments

12 comments on “TOP 6 VING’AMUZI BORA NA MAARUFU VYENYE  WATEJA WENGI NA MATUMIZI MAKUBWA  YA KILA SIKU NCHINI TANZANIA ”
 1. Thanks in favor of sharing such a fastidious idea, article is pleasant,
  thats why i have read it fully

  Like

  1. Thanks indeed , That’s very Awesome for us when we feel that y’all supporting Us .Thank ya once again 마음수련 대학생캠프

   Reply on: 마음수련 대학생캠프
   Sender: NICOLE Jr
   From: Nijuzepedia.com

   Like

 2. It’s in fact very complicated in this active life to listen news on Television, therefore I just use internet for that reason, and obtain the most recent information.

  Like

  1. Yeah Cara ! That’s somethin’ many other folks preferrin’ nowdays all what we coulda say is thanks for ballin’ with us and we gonna make sure that you gon’ feel internet is safe home for ya !

   Like

 3. Hi I am so thrilled I found your webpage, I really found you by mistake, while I was researching on Yahoo for something else, Regardless I am here now and would just like to say thanks a
  lot for a marvelous post and a all round exciting blog (I also
  love the theme/design), I don’t have time to look over it
  all at the moment but I have book-marked it and also added your RSS feeds, so when I have time I
  will be back to read a great deal more, Please
  do keep up the awesome work.

  Like

 4. Hi I am so excited I found your web site, I really found you by error,
  while I was researching on Yahoo for something else, Anyways I am here now and would just like to say cheers for a marvelous post and a all round
  interesting blog (I also love the theme/design), I don’t have time to read it
  all at the minute but I have book-marked it and also included your RSS feeds,
  so when I have time I will be back to read a great deal more, Please
  do keep up the great work.

  Like

  1. You know wha Yang??!! we always workin’ hard just to make sure that we get great and good response from people like you who always supporting Awesome things ! I know we still have gotten great job thru all tha way to the top but if you gonna keep lookin’ over our updates thinkin’ we gonna done all ASAP ! THANK YA SO MUCH

   Like

  1. YOU AIN’T HAVE TO WORRY ABOUT IT BUDDY !

   Like

  2. We Always there Pantangan ! Thank you lotta

   Like

 5. He estado explorando un poco por posts de alta calidad o entradas en webs sobre estos contenidos. Explorando en Google por fin encontré este blog. Con lectura de esta articulo, estoy convencido que he encontrado lo que estaba buscando o al menos tengo esa extraña sensacion, he descubierto exactamente lo que necesitaba. ¡Por supuesto voy hacer que no se olvide este blog y recomendarlo, os pienso visitar regularmente.

  Saludos

  Like

 6. 保育士が職場を変えることを思うようになったら、保育士資格保有者専門の転職サポートサイトをフル活用したほうが良いです。

  Like

Leave Comment / Toa Maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s