TOP 5 MATAJIRI WAKUBWA WA AFRIKA MASHARIKI

UTAJIRI ni ndoto ya kila mtu aliye chini ya jua lakini wengi wetu atujui vitu ya kuzingatia ili kutimiza hii ndoto.Jitihada,umakini na bidii ni vitu vya muhimu wanavyo zingatia matajiri wakubwa duniani.Elimu,ushirikiano na kujali ni vichocheo vya utajiri mkubwa duniani.

MATAJIRI ni watu wenye ushawishi,pesa nyingi na maamuzi juu ya nchi zao.Je unawajua watu hao pande za Afrika Mashariki?fatilia orodha hii kuwajua.


#5

SAIDI SALIM BAKHRESA


Nchi:Tanzania

Utajiri:$ milioni 575

Chanzo:Bakhresa Group of companies

Kitaifa: #3

Kibara: #47

Kuzaliwa: 1949,Zanzibar

Uraia:Mtanzania

Huku akiwa mwenyekiti na muanzilishi wa Bakhresa Group of companies.Alianza na mgahawa mdogo miaka ya 1970 na kuwa mfanyabiashara mkubwa sana baada ya miaka 30 .

Tajiri huyu mwenye maono na ujuzi wa kuongoza ndo vitu vilivyo mfanya afike hapo alipo.Akiwa na miaka 14 aliacha shule na kuanza kuuza mchanganyiko wa viazi vitamu na baadae aliendelea na kuja kuwa tajiri mkubwa Afrika.Huyu ndiye bakhresa


#4

BHIMJI DEPAR SHAH


Nchi:Kenya

Utajiri:$ milioni 700

Chanzo:BIDCO Group of companies

Kitaifa: #1

Kibara: #38

Kuzaliwa: 1931,India

Uraia:Mkenya

Bhimji shah ni mfanyabiashara ,mwana mapindizi wa viwanda na mjasiriamali wa Kenya.Akiwa muanzilishi na mwenyekiti wa BIDCO Group of companies ikiwa ni biashara ya familia na huku ikiwa na viwanda zaidi ya nchi 13 Afrika.Ali orodheshwa  kuwa miongoni mwa matajiri wakubwa zaidi nchini Kenya na jarida la forbes mwaka 2014.


#3

ROSTAM AZIZI


Nchi:Tanzania

Utajiri:$ bilioni 1

Vyanzo:Vodacom Tanzania,Caspian mining na Majengo

Kitaifa: #2

Kibara: #32

Kuzaliwa: 1964,Tanzania

Uraia:Mtanzania

Rostam Azizi ni mwanasiasa,mfanyabiashara,mjasiriamali na mwanauchumi wa Tanzania alitajwa na gazeti la forbes kuwa ni mtanzania wa kwanza kuwa bilionea mwaka 2013.Akimiliki majengo dubai na oman,makampuni na mgodi anashika namba tatu katika hii orodha huku akiwa na utajiri wa dollar bilioni 1 sawasawa na Trilioni 2 za kitanzania.


#2

SUDHIR RUPARELIA


Nchi:Uganda

Utajiri:$ bilioni 1.1

Chanzo:Ruparelia Group of companies

Kitaifa: #1

Kibara: #27

Kuzaliwa: 1956,Uganda

Uraia:Mganda

Akiwa mwenyekiti na mmiliki wa hisa katika ruparelia group huku uwekezaji wake ukiwa katika huduma za kibenki,mifuko ya jamii,elimu ,majengo na mahoteli.Mganda huyu ana utajiri wa dollar bilioni 1.1 sawasawa na Trilioni 2.2 za Tanzania.

Baada ya kufukuzwa na Idi Amini katika utawala wake na kuelekea uingereza .Walilejea mwaka 1985 huku sudhir akiwa na akiba ya dollar 25000 sawasawa na milioni 50 alizopata kupitia kazi mbalimbali .Ruparelia aliwekeza pesa hizo na baadae kuja kuwa tajiri mkubwa sana Afrika.


#1

MOHAMMED DEWJI


Nchi:Tanzania

Utajiri:$ bilioni 1.4

Chanzo:METL Group of companies

Kitaifa: #1

Kibara: #16

Kuzaliwa: 1975,Tanzania

Uraia: Mtanzania

Mohammed akiwa Raisi na Mkurungenzi Mkuu wa METL group ana shika namba moja katika orodha hii ya matajiri wakubwa Afrika Mashariki.Baada ya kumaliza masomo yake ya Bachelors in International Business and Finance mwaka 1998 Georgetown University Washington D.C,Marekani alilejea Tanzania na kuchukua mikoba ya baba yake katika biashara zao za familia huku utajiri wake ukiwa dollar milioni 40 na kupeleka mpaka leo hii utajari wa dollar bilioni 1.4 .

Zingatia

Orodha hii ilitolewa na jarida la forbe la Marekani 2017.

Advertisements

Leave Comment / Toa Maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s