TOP 5 MALLS KUBWA NA MAARUFU  AFRIKA MASHARIKI. 


MALLS haya ni maduka makubwa na ya kisasa ambayo watu huenda kufanya manunuzi mbalimbali. Uwepo wa malls kwenye mji au nchi husika huchukuliwa kama kitega uchumi na moja ya vitu vinavyoonyesha maendeleo ya sehemu au mji husika.

Afrika Mashariki haiko nyuma katika suala la malls maana kwa miaka ya hivi karibuni wakazi wa ukanda huu wameshuhudia ujenzi wa malls kubwa na za kisasa katika miji mbalimbali. Orodha hii inaweza kutegua kwa kushirikiana na wewe kitendawili cha Malls zipi maarufu na kubwa zaidi hapa Afrika Mashariki.

Orodha hii inazingatia umaarufu na ukubwa wa mall husika.

 

 
#5.


Nchi: Tanzania

Mji: Dar es salaam

Mtaa: Mlimani

Ilifunguliwa: Novemba 2006

Ukubwa: Mita za mraba 19,000

Ukubwa kitaifa:  #2Hii ndio mall Kongwe yumkini kuliko zingine kwenye orodha hii.  Ikiwa maarufu na inayosifika kwa kuwa na Cinema yenye “big screen”  kubwa kuliko zote kwenye ukanda wa Afrika mashariki.

Imepakana na chuo kikuu cha dar es salaam . Mall hii imekuwa ikiendelea kutoa huduma nzuri kwa muda mrefu kwa wakazi wengi wa dar es salaam na miji mingine ya jirani huku ikiwa ndio Mall ya kwanza kufunguliwa nchini Tanzania.


 

#4.


Nchi: Uganda

Mji: Kampala

Mtaa: John Bahiha

Ilifunguliwa: 2011

Ukubwa: Mita za mraba 35,000

Ukubwa kitaifa: #1

 

 

Hii ndio mall kubwa zaidi nchini Uganda. Mall hii ni maarufu kwa mwonekano wake mzuri wa ndani na nje.

Mall hii inajitahidi sana kwa kuwa na eneo kubwa la maegesho ya magari (400+) na shughuli zingine za shopping.

Kila mpenda manunuzi maeneo ya jiji la kampala na maeneo ya jirani sehemu ya kwanza kufikiria huwa ni hii mall kubwa nzuri na ya kisasa.

Ukiongelea na kutaja mall zenye hadhi ya juu tafadhali usisahau the Acacia mall.

#3


Nchi: Tanzania

Mji:  Mwanza

Mtaa: Ghana

Ilifunguliwa: 2015

Ukubwa: Mita za mraba 35,500

Ukubwa kitaifa:  #1

Mmiliki: 

 

 

The rock city mall hii ndio shopping mall kubwa zaidi kuliko zingine zote nchini Tanzania huku ikibahatika kuwa kwenye jiji lenye location nzuri zaidi ukanda wa Afrika Mashariki jiji la Mwanza.

Kabla ya mwaka 2016 Mall hii ndio ilikuwa kubwa zaidi Afrika Mashariki.

Ni mall maarufu sana ukanda wa Afrika mashariki huku ikiwa ndio mall iliyodizainiwa vizuri kuliko zingine.Mwonekano wa jengo lake husadifu Uzuri wake huku ukiwakilisha samaki maarufu kutoka jijini Mwanza Sato & sangara. 

Kwa kigezo cha ukubwa wa eneo lote la mall Rock city mall ndio kubwa zaidi Afrika Mashariki ikiwa ina maeneo makubwa matatu, eneo la watoto,maegesho na maduka huku eneo la maduka likiwa limefanisiwa kwa namna ya kipekee sana,  Mall ina ghorofa 5 kwenda chini na ghorofa 4 kwenda juu ya usawa wa ardhi. Kwa vitu hivi vinadhihirisha njisi gani mall hii ni  nzuri sana yumkini kuliko zote Afrika mashariki.
#2


Nchi: Kenya

Mji: Nairobi

Mtaa: Tusker village

Ilifunguliwa: 2015

Ukubwa: Mita za mraba 59, 500

Ukubwa kitaifa:  #2

 

 

Hii ni mall kubwa sana na maarufu iliyopo jijini Nairobi nchini kenya.  Mall hii ina ukubwa wa kutosha na wakuridhisha.  Mall hii haihitaji maelezo mengi kuelezea ubora na ukubwa yake.

Ikiwa ina rate ya nyota 4.5 hii humanisha uwezo mkubwa mall hii iliyonayo.
Ina maduka makubwa zaidi ya 100 ina maegesho ya magari mengi.  Hii ni mall maarufu na kubwa Afrika mashariki.

 

 

 

#1.

Nchi: Kenya

Mji: Nairobi

Mtaa: 

Ilianzishwa: 

Ukubwa: Mita za mraba 65,000

Ukubwa kitaifa:  #1

Mmiliki: 

 

Hii ndio mall kubwa zaidi Afrika mashariki na kati. Ikiwa ipo kwenye viunga vya jiji kubwa zaidi nchini kenya Nairobi. 

Hili halihitaji maelezo mengi maana kwa hivi sasa Afrika mashariki na kati hakuna mall kubwa ya kushinda Two livers licha ya kusua sua kuanza kutoa huduma rasmi.

Mall ya kisasa kabisa huku ikiwa na  mradi wa Solar enegy kubwa sana barani Afrika. Mall hii bila ubishi inafaa kuongoza orodha hii.

 


UJENZI WA SHOPPIN’ MALLS NI KITU KIZURI CHENYE MATOKEO CHANYA KWENYE UCHUMI LAKINI INATUPASA KUFANYA KITU CHA ZIADA.

WAFANYABIASHARA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI INATUBIDI TUWE WAMILIKI WA MADUKA MAKUBWA (STORES)  mfano: Kenya wamekuwa wamiliki wa store ni mfano mzuri wa kuigwa.  Na w wakazi wa Afrika mashariki tusiishie kuwa watazamaji tununue vitu tuunge mkono hizi malls zetu>>>>>>>>>>>>>>


#**** ::ORODHA KWA NAMBA::****#

#

  1. Two livers mall
  2. The garden city mall
  3. The Rock City mall
  4. The Acacia mall
  5. Mlimani city mall

 USISAHAU KUTOA MAONI KUHUSU ORODHA HII NA NYINGINE.

MAANA

Wewe ni sehemu ya Www.Nijuzepedia.com Toa maoni yako na share na wenzio

Advertisements

Leave Comment / Toa Maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s