TOP 10 MAGARI YA KIFAHARI NA YENYE BEI KUBWA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI

TUKIONGELEA magari maarufu na ghali duniani ni zaidi ya usafiri.Ujuzi,umakini na ufundi wa hali ya juu ndio unapelekea magari haya kuwa ya ghali zaidi duniani.Uwezo,ubora na upekee ndo unafanya magari haya kupendwa zaidi na watu wenye pesa duniani.

Ni magari ambayo nchi zinazo endelea hayapatikani,Ni magari yanayohitaji barabara zilizo bora,Ni magari yanayohitaji mtaji mkubwa kwenye uzalishaji wake. Ni magari ambayo uzalishwaji wake ni mdogo sana duniani.

Je unajua ni magari yapi hayo?!   Fuatilia orodha hii kujua na kutambua magari hayo.
#10


Mzalishaji:    Koenigseg

Nchi:    Sweden

Uwezo:     1500 ph

Spidi ya juu:    Mile 248 kwa saa

Bei:    Sh. Bilioni 4

 

Inajulikana kwa jina lingine kama Mclaren P1 gari hili ambalo linauzito wa 3240 lbs uwezo wa injini twin-turbo 5.0-liter V8 na betri ya 4.5 Kwh ni gari imara na bora sana linalo zalishwa sweden.Gari hii pia inauwezo wa kutoka spidi 0 mpaka 60 kwa sekunde 2.8 na spidi 0 mpaka 186 kwa sekunde 10.6 ni gari inayoendana na bei yake.
#9

Mzalishaji:     Koenigsegg

Nchi:     Sweden

Uwezo:     1341 hp

Spidi ya juu:     Mile 250 kwa saa

Bei:    Sh. Bilioni 4

 

Gari hili ambalo lilivunja rekodi ya mashindani ya magari kwa kumaliza ndani ya dakika 2:17.57.Ni gari bora sana huku ikiwa na uwezo wa injini turbocharged 5.0-liter V8 na uzito wa 2800 lbs ni gari imara na yenye uwezo mkubwa sana.
#8

 

Mzalishaji:     Bugatti Automobiles S.A.S

Nchi:      Ufaransa

Uwezo:     1500 ph

Spidi ya juu:    Mile 261 kwa saa

Bei:    Sh.Bilioni 5

 

 

Gari hii inayoweza kutoka spidi 0 mpaka 60 kwa sekumde 2.5 ikiwa na uzito wa kilo 1995 na uwezo wa injini quad-turbocharged 8.0-liter W16 ni gari ya kipekee na ghali sana kutokana na uwezo wake.Kampuni ya magari aya imezalisha na kuuza magari 500 tu.

Gari hili linawateja wengi nchini marekani hasa kwa watu maarufu wenye kiasi kikubwa cha pesa na wanaotaka kuonekana tofauti.

#7

Mzalishaji:   Ferrari

Nchi:    Italia

Uwezo:     740 hp

Spidi ya juu:    Mile 200 kwa saa

Bei:    Sh. billion 5

 

 

Ferrari F60 America ikipewa uwezo na injini yake ya F12’s mighty 6.3 liter V12 ni gari lenye uwezo mkubwa.Huku ikiweza kutoka spidi 0 mpaka 62 kwa sekunde 3.1 .Gari hii ni bora na yakifahari sana.
Watu wenye pesa nyingi huwanunulia watu wanaowapenda gari hili maeneo ya Ulaya na Marekani.

 #6


Mzalishaji:    Pagani Automobili S. P. A

Nchi:    Italia

Uwezo:    730 hp

Spidi ya juu:    Mile 238 kwa saa

Bei :    Sh. billion 5.2

 

 

Ikiwa na uzito wa kilo 1697 huku kampuni ikiwa imezalisha magari 100 tu ya aina hii na uwezo wa injini ukiwa biturbo V12 ikizalishwa na mercedes ni gari bora na ghali sana ambalo linaweza kutoka spidi 0 mpaka 60 kwa sekunde 2.8 .

Gari hili  linapeleka sifa kubwa sana kwa nchi ya Italia ambayo imeonekana kujihusisha zaidi na utengenezaji wa magari ya kifahari kama hili.
#5


Mzalishaji: Ferrari

Nchi:      Italia

Uwezo:    562 hp

Spidi ya juu:     Mile 202 kwa saa

Bei:    Sh. billion 6

 

Huku ikiwa na uwezo wa injini 4.5-liter V8 na uwezo wa kutoka spidi 0 mpaka 60 kwa sekunde 2.8 ni gari ya ghali sana kutoka italia ambayo imebuniwa na Pininfaria.Gari hii ni bora sana  na inayo milikiwa na watu wachache sana duniani.
#4


Mzalishaji:    Bugatti Automobiles

Nchi:    Ufaransa

Uwezo:    1200 hp

Spidi ya juu:    Mile 268 kwa saa

Bei:     Sh. billion 6.8

 

 

Gari hii ilio buniwa na Jozef Kaban ikiwa na uwezo wa injini 8.0-liter W16 na uzito wa 1106 pound ndo vinavyo pelekea gari hii kuwa ya kasi zaidi duniani.Pia ni gari inayo pendelewa kutumiwa na watu maarufu duniani hasa mwanamziki wa marekani.
#3


Mzalishaji:   W Motors

Nchi:    United Emirates Arab

Uwezo:    770 hp

Spidi ya juu:    Mile 240 kwa saa

Bei:    Sh. billion 6.8

 

 

Uwezo wa injini 3.7-liter twinturbo na ikiweza kutoka spidi 0 mpaka 62 kwa sekunde 2.8 sifa hizi ndo vinaifanya nchi tajiri Abu Dhabi kutumia gari hii kama gari za polisi.Imeonekana pia kwenye picha ya furious 7 na game mbalimbali kama Asphalt 8:Airbone,Forza motorsport 6 na GT Racing 2.Kwahiyo ukiwa jambazi pande za Abu Dhabi kuwa makini.
#2


Mzalishaji:   Lamborghini

Nchi:    Italia

Uwezo:     740 hp

Spidi ya juu:   Mile 221 kwa saa

Bei:    Sh. billion 9

 

Veneno ikiwa ndo gari inayo pendwa zaidi na matajiri wakubwa duniani ni gari nzuri na bora sana.Yenye uwezo wa injini 6.5-liter V12 na uzito wa 3278 pound huku ikiweza kutoka spidi 0 mpaka 60 kwa sekunde 2.9.Gari hii ni maarufu sana kutokana na teknolojia iliyotumika kutengeneza ya Advanced Array of Racing Technology na ikipelekea kuwa gari ghali sana duniani.

 

#1


Mzalishaji:    Koenigsegg

Nchi:   Sweden

Uwezo:   1004 hp

Spidi ya juu:    Mile 254 kwa saa 

Bei:     Sh. bilioni 9. 6 

 

CCXR Trevita ni gari inayo zalishwa sweden ikiwa na uwezo wa injini 4.7-liter twin supercharged V8 .Gari  hii ambayo ni ghali zaidi kuliko zote duniani huku ikiweza kutoka spidi 0 mpaka 62 kwa sekunde 2.9.Inashika namba moja kwenye orodha hii na tunzo moja ilioyo ipata mwaka 2009 ya best performing green exotic.Gari hii inamilikiwa na watu wawili tu duniani ambao ni Floyd Myweather na Hans Thomas Gross.

 

 


#

UNA MPANGO WOWOTE WA TENGENGENEZA AU KUMILIKI GARI KATI YA HAYA ????? !!!!!!! 

NCHI INAKUTEGEMEA WEWE KAMA FUNDI GARAGE AU DEREVA FANYA MAMBO BASI MSIISHIE KUAGIZA,, TUNATAKA MUANZE KUTENGENEZA YA KWENU
Wewe ni sehemu ya www.Nijuzepedia.com

Toa maoni na share na share na wenzio

 


Advertisements

Comments

One comment on “TOP 10 MAGARI YA KIFAHARI NA YENYE BEI KUBWA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI”
  1. If you want assist handling protection or taking good care of the ultimate battle, then just appear below.

    Like

Leave Comment / Toa Maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s