TOP 10 BRAND ZA SMARTPHONES MAARUFU NA ZINAZOUZIKA ZAIDI DUNIANI. 

Unapozungumzia Smartphones  kwa hivi sasa si jambo geni miongoni mwa watu wengi duniani kote.

Smartphones  ni simu zenye uwezo mkubwa kuanzia kimatumizi na vitu hasa vinanvyounda simu hizi, Huweza kufanya mambo mengi kwa muda mmoja.

Kama zilivyo bidhaa nyingine tunazidi kushudia ongezeko kubwa sana la Kampuni mbalimbali kutoka nchi tofauti kote duniani zikitengeneza smartphones nyingi na nzuri kila kukicha.       Kutokana na matumizi,  imani kwa wateja pamoja na umakini wa kampuni husika husaidia  sana kufanya Smartphones za kampuni husika kuwa maarufu sana na kutengeneza jina duniani kote.
Hii ni orodha ya Kampuni 10 ambazo smartphones zake ni maarufu sana na zenye soko kubwa zaidi kuliko zingine.

#10.


OS: BlackBerry os, Android

NchiCanada

Makao makuuOntario, Canada

MmilikiBlack Berry Lmited

Mwanzilishi wa kampuniMike Lazaridi

Hizi ni smartphones ambazo kwa mara ya kwanza ziliingizwa sokoni January mwak 1999.  Black berry tangu itambulishe sokoni imekuwa brand maarufu na yenye wateja dunia nzima ingawa kwa miaka ya hivi karibuni kampuni imepata ushindani wa hali ya juu kutoka kwa smartphones zinazotengenezwa na kampuni zingine.

Ulinzi wa simu (cellphone’s security) ambao ni wa hali ya juu sana uliowashawishi hata Hilarry Clinton na rais mstaafu wa Marekani Barrack Obama na wengine wengi, Ilipelekea Smartphones hizi huuzika na kuwa maarufu sana.

 
#9.


OSAndroid

NchiMarekani

Makao makuuSchaumburg Illinois U. S

Kampuni ilianzishwa: 1928

Utajiri wa kampuni$ 13.501 billions

Motorola ni kampuni ya vifaa vya electronics ambayo imejizolea umaarufu mkubwa kote duniani hasa kwa upande wa simu.  Kampuni hii huzalisha smartphones bora zenye kiwango cha kimataifa huku ikiwa imepata wateja kila kona.

Kampuni hii miaka ya hivi karibuni imeingia ubia na Kampuni ya vifaa vya electronics ya LENOVO.  Smartphones za motorola ni nzuri sana na zina kiwango kinachoaminiwa na wengi duniani.

 

 

#8.

OS: Android, window. 

Nchi: Taiwan

Makao makuuNew Taipei,  Taiwan

MmilikiHtc corporation

Kampuni ilianzishwa: Mwaka 1997

Mapato : Taiwanese dollar billion 135

UtajiriTaiwanese dollar billion  145

Soko:  Dunia nzima

******************

Htc hii ni kampuni na brand maarufu sana kwenye ulimwengu wa smartphones.  kwa ubora na matumizi yenye uwezo wa hali ya juu., brand hii imezidi kujizolea umaarufu na soko kubwa duniani licha ya matatizo ya kushuka kwa mauzo ya  hisa zake sokoni kwa kiwango kikubwa sana cha asilimia 90% toka mwaka 2011.
Lakini hili halijazuia kipato cha kampuni kukua siku hadi siku maana kwa kutegemea Tablets na smartphones kampuni inazidi kukuza kipato chake.

 

 

#7.


OSAndroid

NchiChina

Makao makuu: Beijing & Noth Carolina


Kampuni ilianziswa: mwaka 1984

Utajiri$ 24.93 billions
MauzoDunia nzima(nchi 160)

Lenovo ni brand maarufu sana kwa hivi sasa hasa kwa wale watumiaji wa personal computers wanaijua sana kampuni hii .  Kampuni hii imepata mafanikio  makubwa kwenye computer mpaka kweye smartphones.    Smartphones za kampuni hii ni nzuri na zinao uwezo mkubwa.

Lenovo ilianza kuzalisha smartphones kwa mara ya kwanza mwaka 2012 mara baada ya kuongoza mauzo nchini China. Kwa saivi kampuni hii inaubia na kampuni ya Motorola na inazidi kutengeneza smartphones nzuri

 

 

 

#6.

OS: Android

Nchi: Japan

Makao makuu:  sony city,  Tokyo

Mmiliki: Sony

Kampuni ilianzishwa: mwaka 1946

Utajiri wa kampuni:  ¥ 8.2 trillions

Mauzo: Dunia nzima

Wafanyakazi: 125, 360

Sony ericcson ni brand ya smartphone inayozalishwa na kampuni maarufu sana ya electronics ya Sony.  Mwaka 2012 sony ericcson ilitajwa kuwa ya nne kimauzo duniani baada ya kuuza Sale Units millioni 9.8.

Brand hii ni maarufu sana na ina soko la uhakika kwa smartphones zake mana inamilikiwa na moja ya kampuni za electronics kubwa sana duniani kampuni ya Sony.

 

 

#5.  


OS: Android

Nchi: Korea Kusini

Makao makuu: Seoul, korea kusini

Mmiliki: LG corporations

Kampuni ilianziswa: mwaka 1947

Utajiri: $ 143 billions

Wafanyakazi: 220,000

 

 

Hii ni brand ya smartphone inayomilikiwa na kampuni maarufu na tajiri sana duniani

LG corporations.  

Kampuni hii tajiri ikiwa ni ya nne kwa utajiri nchini Korea Kusini hutengeneza smartphones bora sana zenye soko kubwa kote duniani.  Smartphones za Lg kwa kila aliyewahi kutumia atakwambia ubora na uzuri wa hali ya juu wa simu hizi.

 

 

 

#4.

OS:  Window

Nchi: Marekani

Makao makuu: Washington D.c

Mmiliki: Microsoft corporation Inc

Kampuni ilianzishwa: mwaka  1975

Mwanzilishi: Bill Gates

Mapato: $ 85. 40 billions

Utajiri: $ 193.69

Soko: Dunia nzima

 

Hii ni brand ya smartphone maarufu sana duniani.  Humilikiwa na kampuni ya Computer Operating system maarufu sana yenye mafanikio makubwa na tajiri Microsoft Corparations Inc.

Smartphones zinazotengenezwa na brand hii zilianza kuzalishwa mwaka 2010 mara tu baada Kampuni ya Nokia kuingia ubia na Microsoft Corparations Inc.  Smartphones hizi zina mwonekano na uwezo mzuri sana kiasi cha kuaminiwa karibu na watumiaji wote wa smartphones duniani.

 

 

#3.


OS: Android & window

Nchi: China 

Makao makuu: Guangdong

Kampuni ilianzishwa: mwaka 1987

Mwanzilishi: Ren zhengfei

Utajiri: $ billion 57.320

Mapato: $ billion 60.840

Soko: Dunia nzima

 

 

Hii ni brand inayozalisha smartphone bora sana duniani kiasi cha kukwea hadi top 3 ya smartphone zenye wateja wengi duniani.

Wengi hususani huku Afrika Mashariki huichukulia brand hii kitoto lakini ukweli Huawei ni brand kubwa sana inayoaminiwa na wateja wengi sana duniani kote.  kwa saivi ndio Brand inayouza smartphome nyingi zaidi China na Amerika kusini.

 

 

 

 

#2

 

OS: Android, Window, Bada. 

Nchi: Korea Kusini

Makao makuu: Samsung city, seoul

Kampuni ilianzishwa: mwaka 1938

Mwanzilishi: Lee Byung Chul

Mapato: $ billion 305

Utajiri: $ billion 530

Soko: Dunia nzima

 
“Weka mbali na watoto”.. Samsung sio brand  ya kitoto.  Hii ndio brand ya smartphone tajiri zaidi duniani. Kampuni yenye mafanikio makubwa sana zaidi ya sana.

Brand hii inaongoza kwa mauzo duniani kwa kigezo cha Units . Inakadiriwa kwa kila mwaka Samsung inauza zaidi ya simu milioni 70 mpaka 85 kila mwaka.  Hili si jambo la mchezo hata kidogo.

Kwa nini samsung sio ya kwanza kwenye orodha hii?!!!!

Soma makala ya Samsung vs I phone Utagundua mambo mengi ambayo baadhi yake ni..

 • SAMSUNG inatoa simu nyingi sana kwa mwaka tofauti na APPLE ambayo mara nyingi hutoa simu 2 tu kwa mwaka mzima.
 • SAMSUNG ni kampuni inayojihusisha na vitu vingi sana ,  Ujenzi (ghorofa refu zaidi duniani) ,  Uundaji (injini za ndege, vifaru vya kijeshi, magari) na vingine vingi sana.

Zaidi ya hayo Samsung ni brand maarufu sana duniani ambayo ina wateja wengi sana kila kona ya dunia. Smartphones zake zinauzika haraka, kwa uhakika bila wasiwasi. Hakuna haja ya kutaja simu za brand hii maana asilimia 75 ya watumiaji wa smartphone wanazijua.  Ukitoa APPLE hakuna kampuni ya kushindana na Samsung.

 

 

 

#1.

 

 

OS:  IOS

Nchi: Marekani

Makao makuu: Cuperitino, California

Kampuni ilianzishwa: mwaka  1976

Waanzilishi

 • Steve Jobs, Steve Woznia,&Ronald Wyne

Mmiliki: Apple Inc

Mapato: $ billion 220.640

Utajiri: $ billion 322.690

Soko: Dunia nzima

Wafanyakazi: 116,000

 

 

Hii ndio brand ya smartphone  inayouza sanaa kuliko zingine duniani kwa hivi sasa. Ubora wa hali ya juu sana wa smartphones za kampuni hii maarufu kama I phone unaendelea kuizolea umaarufu na sifa kampuni hii ya kimarekani ambayo imetajwa na Google kama brand maarufu zaidi kwa hivi sasa.

I phone sio simu ya kawaida kama mtu aliyezoea kutumia samsung na simu zingine ambavyo anaweza kusema. Hebu tazama sifa hizi mbili za pekee ndo uamini kuwa simu sio kupiga na kuandika message.

 • ULINZI.  Ukinunua Smartphone ya Apple ni sawa na mtu aliyenunua gari likasajiriwa hata endapo likiibiwa lijulikane kiurahisi.   Iphone haiflashiwi.!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 • UFANYAJI KAZI. Kama unajua maana ya kuwa na smartphone ni lazima utakuwa na mipango ya kumiliki smartphone ya Apple, maana ndio simu yenye Proceser kubwa zaidi duniani, Storage kubwa kuliko smartphone zingine.  IOS kama operating system ya smartphones hizi ndio yenye nguvu sana kuliko zingine. Na mengine mengi.

Brand ya Apple ni maarufu sana na haihangaiki kutafuta wateja.   Ndio kampuni pekee yenye jeuri ya kutangaza tarehe tu ya kutoa toleo la bidhaa zao na wateja kufunga safari toka nyumbani kupanga foleni na kusubiri bidhaa za APPLE.


Swali :   USHAWAHI KUSIKIA KITUO CHA REDIO AU TV KIKIRUSHA TANGAZO LA    I-PHONE   ??????? ?!!!!! 

Toa jibu>>>>>>>>

maana


wewe ni sehemu ya www.Nijuzepedia.com Toa Maoni na share na wenzako

Advertisements

Comments

2 comments on “TOP 10 BRAND ZA SMARTPHONES MAARUFU NA ZINAZOUZIKA ZAIDI DUNIANI. ”
 1. baraka walesa says:

  Apple maarufu kama i phone Naipenda licha ya kutumia blackberry kwa mda.

  Liked by 1 person

  1. YEAH NI NZURI HUSUSANI INAPOKUJA KWENYE SUALA LA MATUMIZI NA MAANA HALISI YA SIMU ,,,, AHSANTE KWA MAONI YAKO Baraka

   Like

Leave Comment / Toa Maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s