Njia 4 rahisi za kupunguza sukari haraka ndani ya saa 48

Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa mbaya sana usio wa kuambukiza. Tatizo hili la kiafya linaendelea kuwatesa watu wengi na kuwaacha bila kujua kipi au tiba ipi sahihi kwa ugonjwa huu.   Tatizo hili limegawanyika makundi makuu mawili la 

 • Tatizo la kupanda kwa sukari mwilini.
 • Tatizo la kushuka kwa sukari mwilini.

Leo tunaangalia namna ya kupunguza haraka sana sukari iliyopanda na kuidhibiti ibakie katika hali ya kawaida huku ukiendelea na matibabu mengine.  Njia hizi zinaaminiwa na wataalamu wengi wa afya kwa kuwa zina matokeo ya moja kwa moja ndani ya muda mfupi…..Ambatana nami uzielewe ;

 

 

#1.  KUNYWA MAJI MENGI.

wadda

Maji yana faida sana nje na ndani ya mwili na hutibu magonjwa mengi sana likiwemo tatizo hili la kupanda kwa sukari. Unapokunywa maji mengi mwili huondoa sukari mwilini kwa njia ya mkojo. Usijali ,ushauri wa wataalamu unadai kunywa birauli 8 mpaka 12 kwa siku moja. Jihurumie kunywa maji mengi bila kipimo na kwa bahati nzuri sana maji hayana madhara yoyote katika mwili wako.

Hivyo kama sukari yako imepanda tafadhari kunywa maji mengi iwezekanavyo  na utaona matokeo ndani ya muda mfupi sana. Cha muhimu baada ya kuanza kunywa maji kumbuka kuwa karibu na kipimo ili kujua kiwango cha sukari mwilini mwako.

 

 

#2.FANYA MAZOEZI.

 

Mazoezi.jpg

Mazoezi yatakusaidia sana kushusha sukari haraka sana ndani ya masaa machache sana.  Mazoezi yanasaidia sana kupunguza vitu mwilini kama vile taka mwili kitu kinachopelekea seli na Insulin  kufanya kazi yake vizuri na kuweza kutumia vizuri sukari iliyopo mwilini . Mazoezi ya kawaida ambayo unayoweza kufanya ili kushusha sukari kwa muda mfupi ni 

 • Kuendesha baiskeli.
 • Kukimbia.
 • Kuogelea.
 • Kutembea umbali wa wastani.
 • Kunyenyua vitu vyenye uzito wa wastani
 • Na mazoezi mengine ya kawaida yasiyochosha sana mwili.

Ukifanya hivi Utapunguza na kushusha sukari katika muda mfupi endapo utajihusisha na mazoezi. Hata baada ya kushusha kiwango cha sukari mazoezi ni kitu muhimu sana kama una tatizo la sukari mwilini.(Ni sehemu ya tiba ya ugonjwa huu). Sijawasahau wale wasio na uwezo wa kufanya mazoezi pindi wanapokutwa na tatizo hili la kupanda kwa sukari. Kama mgoniwa ana tatizo la kutoweza hata kutembea wala kunyenyuka … Mpeni maji ya kutosha huku mkiangalia taratibu zingine za matibabu , Atakuwa vizuri tu..

 

 

#3. ACHA KABISA KUTUMIA  VINYWAJI NA VYAKULA VYENYE SUKARI.

 

 

sugar foods.jpg

Vyakula na vinywaji vyenye sukari kwa muda sukari itakuwa imepanda hutakiwi hata kufikiria kuhusu vitu hivi, kwa sababu  vitazidi kuongeza ukubwa wa tatizo. Zingatia sana hili.  Ukiepukana na matumizi ya vyakula hivi itakusaidia yafuatayo

 • Itapunguza hatari ya kupata mshituko wa moyo
 • Itasaidia ubongo kufanya kazi vizuri.
 • Itapunguza kiwango cha shinikizo la damu  

Hizo ni baadhi ya faida ya kuacha vyakula na vinywaji vya sukari. Kwa hayo na mengine  utapunguza na kushusha kiwango cha sukari mwili kwa muda mfupi. Amini.

 

 

 

#4. PUNGUZA MSONGO WA MAWAZO (STRESS).

Punguza mawazo.jpg

Kuwa na msongo wa mawazo ni kitu kibaya sana kwa mtu mwenye tatizo la kushuka au kupanda kwa kiwango sukari mwilini. Msongo wa mawazo ni hatari sana kwa sababu hii hapa;

Mwili una homoni zinazoitwa Glucagon na Cortisol. Unapokuwa na  msongo wa mawazo homoni hizi hupandisha kwa haraka sana kiwango cha sukari mwilini. Hivyo unahitaji kujiepusha na msongo wa mawazo mambo yatakwenda kinyume yaani sukari itapungua haraka sana. Unatakiwa uzijue baadhi ya njia zitakazo kufanya uepukane na msongo wa mawazo zikiwemo zifuatazo;

 • Pumua pumzi ndefu (deep breath)  kwa dakika 5 na Muuombe MUNGU akusaidie .
 • Tulia tafuta sehemu au kitu cha kukupa joto kwenye shingo au mikono kwa dakika.10.
 • Cheka kwa sauti na kwa furaha huku ukiwa karibu ndugu na marafiki.(Laugh Outta Loud)
 • Acha kabisa  kufikiria kabisa kuhusu kifo au hatima yako ( Usihofu ndugu haijalishi ukiwa na Ugonjwa huu kwamba Maisha yako yako hatarini)    USIAMINI MAMBO KAMA HAYO KAMWE !!!!

 

KWA UFUPI

 1. KUNYWA MAJI MENGI.
 2. FANYA MAZOEZI.
 3. ACHA KULA AU KUNYWA VITU VYENYE SUKARI.
 4. EPUKA MSONGO WA MAWAZO .

HIZO NI NJIA RAHISI AMBAZO KILA MTU ANAWEZA KUZITUMIA KUEPUKANA NA TATIZO HILI .USIKOSE KUJUA #Vyakula vinavyofaa kutumiwa na watu wenye tatizo la sukari na shinikizo la damu. 

 

 

#PUNGUZA STRESS MAMBO SIO MAGUMU KIASI HICHO.

banana_car_pic_large_fathers-day-blue-mountain.jpg

.Wewe ni sehemu ya www.NIJUZEPEDIA.COM Toa maoni yako na share na wenzio 

 

Advertisements

Comments

2 comments on “Njia 4 rahisi za kupunguza sukari haraka ndani ya saa 48”
 1. Quality Post – naturally refreshing to find articles that aren’t just regurgitating what we’ve already seen. Hope your blog gets alot more
  discussion. Anyway, doing you a favor by sharing this on my Twitter.
  Type 2 Diabetes won’t be keeping me down 🙂

  Like

  1. Let’s email you friend ….let’s tryna workin’ together with you!

   Like

Leave Comment / Toa Maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s