Top 10 Matunda rahisi kupatikana na yenye faida kubwa sana kwa Afya yako.

Suala la Afya bora  ni suala la muhimu sana katika Maisha ya kila mmoja wetu na taifa kwa ujumla. Bila afya hakuna furaha,amani wa shughuli yoyote ile ya maendeleo.Afya ndio msingi wa maisha yetu ya kila siku.Siku hizi si ajabu sana kusikia au hata kushuhudia watu wengi wakisumbuliwa na matatizo mengi sana ya kiafya, suala hili linachangiwa na mambo mengi hali ya mazingira au tabia za watu.

Upuziaji wa matumizi ya matunda na mboga mboga unachangia kwa kiasi kikubwa matatizo ya mengi ya kiafya. Matunda ni moja ya zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu binadamu tuliopewa japo tunaidharau licha ya faida yake katika maisha yetu.

Kuna sababu kadhaa za kwa nini watu hawatumii matunda mara kwa mara , baadhi ya hizo ni Kutokujua faida ya matunda kiafya, na Ukosefu wa uwezo wa kumudu gharama za kula matunda mara kwa mara.  Ikiwa wewe ni miongoni mwa watu wanaoshindwa kutumia matunda kwa moja ya sababu hizi basi taarifa hii inakuhusu na uyajue matunda yenye gharama nafuu sana wakati huo huo yakiwa na faida tele kiafya kwa mwili wako.

#1.

MACHUNGWA

grapefruit

Haya ni matunda matamu sana ,rahisi sana kupatikana na yenye faida nyingi mno kwa afya yako.Matunda hayab hupatikana kwa wingi bila gharama kubwa  mfano kwa wale waliofika Morogoro na Tanga  wanajua uwingi wa matunda haya. kama hujui tazama virutubisho muhimu sana viliyomo katika machungwa.

 • Vitamin C   __________________ 93%
 • Fiber             __________________ 13%
 • vitamini B1 __________________  9%
 • Pottasium   __________________  7%
 • Calcium      ___________________  5%

Na virutubisho vingine vingi sana huku  vikiwa na faida muhimu zaidi ikiwemo:

 • Vitamic C ya machungwa husaidia kuimarisha  ulinzi wa Antioxidant na ulinzi dhidi ya magonjwa
 • Machungwa husaidia kuzuia ugonjwa wa mawe katika figo(kidney stones)
 • Machungwa huzuia kansa na vidonda vya tumbo
 • Machungwa husaidia na kuboresha  afya ya mfumo wa upumuaji.

Yapo mengi na faida nyingi sana za machungwa …Machungwa sio gharama ,ni rahisi kupatikana yatumie mara kwa mara uone faida yake kwa afya yako.

#2.

NANASI

pineapple.jpg

Nanasi ni tunda maarufu na linalopatikana karibu maeneo yote kwa urahisi.Tunda hili lina virutubisho vya kusaidia ubora wa afya yako.Baadhi ya faida ya nanasi ni;

 • Husaidia kwa kiasi kikubwa ulinzi wa mwili.
 • Husaidia seli na tishu mwilini kwa vitamini c iliyomo katika tunda hili suala linalopelekea kujengwa kwa sehemu muhimu ya protini iitwayo COLLAGEN ambayo huimarisha mishipa ya damu,ulinzi wa ngozi,ogani na mifupa mwilini.
 • Husaidia sana kukukinga na kansa kwa kuupatia mwili wako vitamini A na C zenye uwezo mkubwa wa kupambana na kansa mwilini.

Nanasi ni tunda lenye faida kubwa sana mwilini mwako hizo ni chache kati ya nyingi, hivyo tumia fursa ya gharama  ndogo ya matunda haya kwa faida ya afya yako.

#3.

PARACHICHI

avocado.jpg

Parachichi ni tunda rahisi sana kupatikana hasa sehemu za baridi. Watu wanaoishi maeneo haya wana ushahidi juu ya hili.Huuzwa nchi nzima kwa bei ndogo na ya kawaida kabisa huku likiwa na faida kubwa sana kiafya.Baadhi ya virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye tunda hili ni;

 • Vitamini K  __________ 26%
 • Folate          __________ 20%
 • Vitamini C __________  17%
 • Potassium  __________  14%
 • Vitamin E   __________  14%
 • Vitamin B5 __________  14%
 • Vitamin B6 __________  13%

Kwa orodha ya virutubisho hivyo  hapo juu Parachichi  litasaidia sana mwili wako kurekebisha msukumo wa damu, Tunda hili lina 77% ya protini kitu kinachofanya tunda hili liwe mmea wenye protini kuliko mwingine wowote ule.Husaidia macho kuona vizuri zaidi, zaidi husaidia nywere na ngozi yako, Na faida nyingine nyingi sana.Hauna budi kutumia parachichi mara kwa mara.

#4.

PAPAI

paw-paw

Papai ni moja ya tunda zuri,tamu likiwa vilevile linapatikana kwa urahisi na gharama nafuu.Kama ulikuwa hujui faida za papai  kwa afya yako ngoja nikuibie siri. Papai ndio tunda lenye utajiri wa madini mengi sana ukilinganisha na matunda mengine pamoja na virutubisho vingine vingi.Baadhi ya faida za tunda hili ni kama vile;.

 • Husaidia sana kupunguza uzito (weight loss), Ikiwa kila nusu kipande kikiwa na Calories 120.Tunda hili ni la muhimu sana kwenye suala la kupunguza uzito …kama unashida ya uzito usiotakiwa tumia tunda hili mara kwa mara litakusaidia sana.
 • Husaidia sana kinga ya mwili kwa zaidi ya 200%.Utajiri wa Vitamini C papai lililonao husaidia kinga ya mwili kuwa imara pindi unapotumia mara kwa mara.
 • Ni tunda nzuri kwa wagonjwa wa kisukari.Papai lina kiwango kidogo cha sukari(8.3 gram kwenye kikombe cha papai zilizokatwakatwa vipande vidogo).Juisi yake ni nzuri sana kwa sukari huku ikiwa  na Vitamini nyingi zenye kusaidia mgonjwa wa sukari kuepukana na magonjwa ya Moyo.

Faida za papai ni nyingi sana ,Husaidia kurainisha na kurinda ngozi,husaidia macho kuona vizuri,huasidia mfumo wa usagwaji wa chakula mwilini n.k, hivyo litumie mara kwa mara.

 

 

#5.

EMBE

mangomangos

Tunda hili ni maarufu na rahisi sana upatikanaji wake huku likiwa na bei ya kawaida sana.Maeneo kama ya mubende, kampala, Tommy, kent,mashamba ya Capsicum ,Embu ishiara ,karurumo,Tabora, Tanga, Morogoro, Kigoma,  na maeneo mengine mengi sana ya Afrika mashariki, tunda hili hulimwa na kustawi kwa wingi sana. Licha ya hilo bado watu wanapuuza kutumia tunda hili kiafya, Ila wewe unatakiwa ujue faida za tunda hili mfano,

 • Linasafisha ngozi, linaimarisha sana  afya ya macho.
 • Lina virutubisho venye Antixiodant vinavyosaidia kukukinga na kansa kwenye mwili wako.
 • Hongeza hamu ya tendo la ndoa  na nguvu za kiume.
 • Kubwa zaidi hukuepusha na ugonjwa wa mshituko wa moyo (heart stroke)

Ni baadhi ya faida chache na muhimu sana kwa ajiri ya mwili wako …. Jenga mazoea ya kula maembe kwenye milo yako na ufurahie afya bora.

 

#6.

NDIZI

banana.jpgNdizi ni tunda maarufu sana  lenye faida tele kwa mwili wako huku likipatikana kwa gharama ndogo na kwa urahisi. Ndizi ina virutubisho vingi venyefaida nyingi sana kwa afya yako ikiwemo.

 • Potassium  ______________   9%
 • Vitamin B6 ______________   33%
 • Vitamin C   ______________    11%
 • Protein       _______________   1.3 grams
 • Fat                _______________   0.4 grams

Na vingine vingi sana kiasi cha kutotaja vyote  huku vikiwa na faida kwa mwili wako kama vile,

 • Kurekebisha kiasi cha sukari mwilini (ndizi ina Kalories 105 pekee).
 • Inapunguza uzito usiotakiwa (weight loss).
 • Potassium iliyopo kwenye ndizi Inaboresha afya ya moyo.
 • Husaidia Insulin na figo kufanya kazi vizuri .

Na faida zingine nyingi sana hupatikana kwa kutumia ndizi mara kwa mara.

 

#7.

TIKITI MAJI

watermelon

Tikiti maji naamini ni tunda linalofahamika na watu wengi sana ,Tunda hili licha ya watu wengi kutokujua lakini lina faida nyingi mno kiasi cha kushauriwa kutumika mara kwa mara na wadau mbalimbali wa masuala ya afya. Hizi ni baadhi ya faida muhimu sana za tunda hili

 • Pamoja na tikiti maji kuwa tamu kwa ladha lakini tunda lina Karolies chache sana (105 Calories), wakati huo huo 92% ya tunda hili ni maji. Kitu hiki kina faida mno kiwenye mwili wako hasa baadhi kazi zile ambazo maji hufanya mwiulini hufanywa na tunda hili.Fibers na Maji ya tunda hili hukupa afya bora wakati huo huo likiwa  na calories.
 • Lina vitamin C , Vitamini A, Vitamin B1, Vitamin B5, Vitamin B6 na virutubisho vingine vingi  vyenye faida nyingi sana kama vile , kukukinga na kasa, kuboresha afya ya moyo,Ni tunda zuri sana kwa afya ya ngozi na nywere n.k .

Litumie mara kwa mara uone faida hizi kwenye mwili wako.

#8.

PASSION 

passion

 

Matunda sio tu mazuri kwa harufu nzuri sana yaliyonayo.LA hasha !!!! Tunda hili linafaida kubwa sana kiafya .Tunda hili lina viritubisho muhimu sana kwa afya ya mwili wako mfano,

 • Energy              ____________   97 kcal
 • kabohydrate   ____________    23.38 grams
 • protini              ____________     2.2 grams
 • Vitamin A        ____________     1274 IU
 • Magnesium     ____________     29 grams
 • Madini chuma ____________     1.6  Milligramu

Na virutubisho vingine vingi sana  vinavyokulinda na kansa, shinikizo la damu na shmbulio la moyo, magonjwa ya macho, Anemia, Ulinzi wa mwili dhidi ya magonjwa na matatizo mengine mengi ya kiafya. USIPUZIE tunda hili lina faida sna kwa mwili wako.

 

#9.

MAPEAZI

pears

Matunda matamu sana na yenye faida kubwa sana kwenye mwili wa binadamu.Tunda hili lina vurutubisho muhimu sana kwa afya kama ifuatavyo;

 • Fiber                 ________________ 23%
 • Copper             ________________  17%
 • Vitamin C        ________________  10%
 • Vitamin K        ________________  9%

Takwimu hizi kwa mujibu wa Orodha ya mfumo wa ubora wa vyakula yaani  Food Rating System Chart huonyesha  matunda haya kuwa %DV  ikimanisha kuwa peazi ndio tunda lenye uwiano sahihi sana wa virutubisho kuliko matunda mengine.

Matunda haya  husaidia sana  mwili wa binadamu kuepukana na magonjwa ya moyo na sukari, Hupunguza hatari ya kupata kansa, na faida nyingine nyingi sana kiafya.

JE WAJUA ?!……… Kwa mujibu wa Shirika la Marekani la udhibiti wa magonjwa U.S Center for diseases control Peazi ndio tunda lenye mzio mdogo kuliko mengine (most low allergy fruit).  Unasubiri lini wakati ushafahamu faida ya tunda hili ?! fanya kulitumia walau hata mara kadhaa kwa kila mwezi, Naongea hivi kwa sababu matunda haya hupatikana kwa wingi katika sehemu na sehemu lakini hii haimanishi kwamba hayapatikani.

 

#10.

TANGO

sliced-cucumber.jpg

Hili ni tunda (Cucumber) sio mtandao maarufu wa kijamii wa “Tango meesenger”. Tunda hili lina faida nyingi mno kuliko unavyoweza kufikiria ! Hebu tazama baaadhi yake >>>

 • Hulinda ubongo ,Tango lina kirutubisho kinachoitwa Fisetin ambacho huupa ubongo afya bora sana, kwa kukusaidia kutunza kumbukumbu,na kuzidisha uhai wa seli mbalimbali kwenye ubongo.
 • Linakulinda na hatari ya kupata kansa, Tunda hili lina Kirutubisho kinachoitwa  Lignans ambacho huweza kukusaidia kuepuka kansa ya maziwa, kibofu, via vya uzazi, vilevile Cucurbitacin  ni kirutubisho muhimu sana kwa ulinzi dhidi ya kansa.
 • Hukupa usafi wa kinywa na hewa toka mdomoni na ulinzi wa kinywa na menoTunda hili linao uwezo mkubwa sana wa kuua bakteria wanaosababisha harufu mbaya ya kinywa na magonjwa ya meno.Hivyo hukuepusha na hatari  za bakteria hatari kwa kinywa na meno yako.
 • Huwafaa  sana wagonjwa wa kisukari.Tango likiwa ni tunda lenye Kalories chacche sana (calories 16 kwa kikombe cha vipande vidogo vidogo)….Hii ni habari njema sana kwa wagonjwa wa sukari kufaidi faida mbalimbali za kiafya zinazotokana na tunda hili bila hofu yoyote ya kupanda au kushuka kwa sukari.

Hizi ni baadhi ya faida nyingi za tunda hili ambalo sio adimu ukiamua kulitafuta utalipata kwa urahisi na gharama nafuu ya kuridhisha.Rafiki yangu usipuzie ni muhimu sana kuzingatia faida zake kiafya.

KWA FAIDA YAKO :

MATUNDA NI CHAKULA KITAMU, CHA GHARAMA NAFUU, RAHISI SANA KUPATIKANA. MUNGU  ALIWAPATIA BINADAMU MATUNDA KAMA DAWA NA CHAKULA CHAO .  NANASI MACHUGWA PAPAI PARACHICHI  NDIZI  TIKITIMAJI na mengine mengi sana husaidia mno kujenga na kulinda afya ya mwili wako , zingatia haya utaishi kwa afya njema.

 

JE  UNAPENDA  HAYA  MATUNDA   ??????!!!!!

 

 

TUAMBIE NA TOA MAONI  YAKO KUHUSU MAKALA HII ULIOISOMA !!!

 

Wewe ni sehemu ya www.NIJUZEPEDIA.com toa maoni na share na wenzako

Advertisements

Comments

12 comments on “Top 10 Matunda rahisi kupatikana na yenye faida kubwa sana kwa Afya yako.”
 1. I am prepared to attempt once again !

  Like

 2. Hello! This post could not be written any better! Reading this post reminds
  me of my old room mate! He always kept chatting about this.
  I will forward this page to him. Pretty sure he will have a good read.

  Thank you for sharing!

  Like

  1. Thank you too and always feel free when you wantta visit us !

   Like

 3. 86Nancee says:

  I see you don’t monetize your page, don’t waste your traffic, you can earn additional bucks every month
  because you’ve got hi quality content. If you want
  to know what is the best adsense alternative, search in google: Mertiso’s tips

  Like

  1. Oooh yeah guess I’mma understandin’ what ya saying famo ! buh can we gon’ have contact for more talks and exchangin’some ideas if not workin’ together ?!

   Like

 4. Chante says:

  I all the time used to read article in news papers but now as I
  am a user of internet thus from now I am using net for posts, thanks to web.

  Like

  1. #Chante …… Thanks and please keep lookin’ forward from our site because we’re goin’ to bribng you great things ever !

   Like

 5. Hey I know this is off topic but I was wondering if you knew of any widgets
  I could add to my blog that automatically tweet my newest twitter
  updates. I’ve been looking for a plug-in like this for quite some time and was hoping maybe you would have some experience with something like this.
  Please let me know if you run into anything. I truly enjoy
  reading your blog and I look forward to your new updates.

  Like

  1. THANK YOU MUCH ….AND PLEASE GET READY FOR NEW GREAT TGHINGS EVER HAPPENED …(TRUST WHAT I’mma saying )

   Like

 6. Filomena Barongo says:

  Asanteni sana

  Like

 7. revise says:

  Good article! We wіll be linking to thiѕ grеat post on our website.
  Keep up the gooԀ writing.

  Like

 8. Ready to gain Instagram followers, quicker then ever?

  Like

Leave Comment / Toa Maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s