TOP 10 LIGI ZA SOKA BORA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI.

Hapa ndipo ulipo ubishi wa wengi hasa kwa mashabiki na wapenzi wa mchezo unaotawala zaidi duniani mchezo wa Soka. Ubora wa ligi huchangiwa na ufatiliwaji wa  mashabiki ,viwango vya wachezaji,ushindani miongoni mwa timu za ligi husika pamoja na ushiriki na ushindani katika mashindano ya kimataifa wa timu za ligi fulani.

UEFA hili ni shirikisho la soka barani ulaya lenyewe hupanga ubora wa ligi zake ambazo ndizo ligi zenye mafanikio zaidi duniani kwa mujibu wa matokeo na viwango vya shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA.          EPL na LA LIGA  ndizo ligi zenye ushindani wa hali juu kiasi cha kuchanganya mashabiki wengi wa soka duniani huku EPL ikiwa ndio ligi maarufu na yenye mashabiki kuliko ligi yoyote ile duniani. Fuatilia orodha hii ikiwa na maelezo ya kutosha kwako wewe mshabiki wa soka kuhusu ligi kumi maarufu na bora zaidi duniani.Karibu…

 

 

#10

MAJOR LEAGUE SOCCER

mls

Hii ni ligi kuu ya soka ya nchi tajiri zaidi duniani Marekani.Imeanza rasmi mwaka 1994 mara baada ya Marekani kuandaa kombe la dunia.Tangu hapo soka imekuwa chanzo cha burudani katika majimbo kadhaa suala liliosaidia ligi hii kukua siku baada ya siku na kujizolea mashabiki wa kweli.Kitu ambacho sio kizuri kuhusu ligi hii ni kwamba ligi hii huchukuliwa na wachezaji wa ulaya kama sehemu ya kumalizia maisha yao ya soka.

Lakini licha ya hayo yote pamoja na utawala wa miaka yote wa mchezo wa kikapu nchini Marekani ligi hii ya soka ni maarufu na bora ikiwa ina timu zenye mafanikio na umaarufu katika bara la Amerika kaskazini kama vile L.A galaxy,New york redbull n.k.

 

 

 

#9

BRAZILIAN SÈRIE A

campeonato_brasileiro_serie_a_0brazil_serie_a_live_streaming

Ligi kuu ya nchi yenye mafanikio makubwa katika soka kuliko nyingine nazungumzia Brazil.Ligi hii ikimeremeta na uzuri wa soka la aina yake linaloitwa samba na mechi zenye mvuto sana huofanya iwe maarufu na bora duniani ingawa kiukweli ubora wa ligi hii unabakia nyuma ukilinganisha na ubora wa ligi za ulaya.Mwaka 2015 mabingwa wa ligi hii timu ya Colinthans ilishinda ligi ikiwa na pointi 81 wakati timu ya mwisho ya Joinville ilikuwa na pointi 31 na kufanya tofauti kubwa sana ya pointi 51 jambo ambalo si zuri kwa ligi bora.

Lakini jambo zuri kuhusu ligi hii ni kwamba shirikisho la soka la Amerika kusini Copa libertores linatambua ligi hii kuwa imekuwa ikitoa angalau timu 4 katika  misimu 3 ya mwisho ya kombe la vilabu vya soka Ameriks kusini.

 

 

 

#8

LIGA ARGENTINA

liga-ar Ligi kuu ya Argentina ni moja ya ligi bora na maarufu duniani kutokana na soka lenye kujaa wachezaji wenye vipaji vya kiwango cha hali ya juu.Unaweza ukasema hii ni ligi bora sana katika bara la Amerika kusini ikiwa ina vilabu kama vile independetienteBoca juniorestudiantes zenye mafanikio ya juu kabisa kwenye kombe la Copa lebertores.kitu kinginze kizuri zaidi ni kwamba tofauti na ligi kuu zingine ligi hii inazo timu 30 zinazoshiriki ligi kuu zikiwa zimegawanywa kwenye makundi mawili ya timu 15 kila moja kitu kinachoifanya ligi hii kuwa bora sana.

 

 

 

#7

DUTCH EREDIVISIE LEAGUE

Eredivisie.jpg

Ligi kuu ya uholanzi hii ni moja ya ligi bora sana ulaya na duniani.Hii ikiwa ni moja ya ligi zenye watani wa jadi wenye ushindani mkali sana timu ya PSV na Ajax .Timu hizi ndizo timu zenye academies bora zaidi duniani zikiwa zinatoa nyota wenye umri mdogo kila kona ya bara la Ulaya. Wachezaji wengi sana wamejifunzia na kukuza viwango vyao katika academies hizi baadhi yao ni  nyota Ronaldo de rima, Ruud van Nistelrooy, van persie, Arjan Rooben na nyota Luis suarez.Hao ni baadhi ya wachezaji nyota waliopitia katika academies hizi. vile vile  ligi hii ndio ligi yenye magoli mengi zaidi kwa kigezo cha uwiano mechi barani Ulaya.

Lakini vitu vibaya kuhusu ligi hii ni kuwa ligi yenye kadi nyekundu kuliko zingine ulaya. Kingine ligi hii imeshindwa kuleta ushindani Ulaya kwani kwa mara ya mwisho timu kutoka ligi hii kushinda ligi ya mabingwa barani ulaya UEFA ilikuwa mwaka 1995 ambapo Luis van gaal aliipatia ubingwa wa nne timu ya Ajax. pamoja na hayo bado ni ligi hii maarufu na bora duniani.

 

 

#6

FRENCH LIGUE 1

ligue_1_34703

Hii ni ligi kuu ya Ufaransa,Ni ligi bora sana na yenye historia ya namna yake.Miaka ya 1990 ligi hii ilikuwa ligi isiyotabirika  na hili lilithibitika mara baada ya ulimwengu wa soka kushuhudia ubingwa wa timu 7 tofauti ndani ya miaka 9 si mchezo. Hii ni rekodi ya aina yake. Lakini Klabu ya olyimpic lyon ilitawala ligi hii kwa ubingwa wa mara 7 mfululizo toka mwaka 2002 mpaka 2008 na baadaye kutokea kipindi kifupi tena cha miaka miine ya kutotabirika kwa ligi hii baada ya kushuhudia ubinwa wa timu 4 tofauti katika misimu miine ya ligi.Tokea hapo ligi hii imetawaliwa na klabu tajiri ya soka ya Paris saint German (PSG).

Ligi hii imejikuta ikipoteza vipaji kwa ligi zingine za ulaya na kukosa ushindani katika mashindano mbalimbali barani ulaya huku PSG ikionekana angalau kuwa na mafanikio.Lakini bado hauna budi kusema LIGUE 1 bado ni ligi nzuri na bora huku ikiwa na mashabiki sehemu mbalimbali duniani.

 

 

#5

PORTUGUESE LIGA

portuguese-primeira-liga.jpg

Ikiwa imetawaliwa kwa muda mrefu sasa na vigogo wawili wa ligi hii timu za Fc porto na Benefica zikiwa ndio timu bora ziadi nchini Ureno kwa kutawala ligi hii toka mwaka 2002 mpaka leo hii na vile vile timu hizi ni  moja ya timu zenye mafanikio makubwa kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa barani ulaya UEFA, Huku kila moja ikishinda kombe hilo mara mbili.

Kama ulikuwa hujui ni kwamba Ligi hii inao ubora sawa kabisa na ule wa ligi kuu ya Hispania lakini tatizo la  ligi hii ni sawa na lile la ligi kuu ya Uholanzi la kukosa uvumilivu na uwezo wa kukaa na wachezaji nyota wenye vipaji badala yake kuishia kuwauza kwa timu za ligi nyingine.Ila ligi hii inatajwa na wadau wengi wa soka kuwa moja ya ligi bora kabisa duniani.

 

 

 

#4

ITALIAN SERIE A

serie-a

Ligi kuu ya Italia maarufu kama seria A ni ligi bora sana na maarufu sana duniani.Ikiwa na timu maarufu na zenye mafanikio tele.Karne moja iliyopita ligi ya Italia ndio ilikuwa ligi bora zaidi iliyokuwa imejaa wachezaji wenye vipaji na viwango vya hali ya juu sana.Mwaka 2007 licha ya kutwaa ubingwa wa UEFA kwa timu ya AC milan na Mwaka 2010 kwa Inter milan kutwaa UEFA ,ligi hii bado imekwama tokea kipindi hicho.Ikishuhudia ushindani mdogo sana huku timu zingine zikizidi kuwa chini ya utawala wa Juventus ambayo mpaka sasa imetwaa taji la ligi mara 5 mfululizo.

Licha ya hayo jambo hili ni la muda tu na watu wanaamini timu kama Fiorentina , AC milan, Inter milan na nyingine zinafanya mikakati ya kurejesha hadhi ya seria A.

 

 

 

#3

GERMAN BUNDESLIGA

bundasiliga

Ushindani, nguvu na ushiriki wa wastani kwa timu ngeni za ligi kuu, yote haya huwakilisha Ligi maarufu na bora duniani ya nchi yenye mafanikio makubwa sana ya soka Ujerumani.Ligi hii ni bora asikwambie mtu ,uuzwaji waki za klabu kwenye matangazo ya televisioni duniani kumezidi kuongeza umaarufu na mashabiki kwa timu za Ujerumani kote duniani.Mbali na hilo Barcelona na Bayern Munich  ndio timu zinaaminika kuwa timu bora zaidi duniani.Ligi hii kwa karne zima imezidi kuwa kivutio cha mashabiki wa kandanda duniani.

 

 

 

#2

SPANISH LA LIGA BBVA

la-ligaHapa ndipo utata mkubwa  ulipo !!! kwa orodha hii kutoka nafasi ya kumi hadi ya tatu hakuna yoyote wa kuhoji kitu chochote lakini siku zote unapozungumzia ligi bora duniani nafasi mbili za juu ndipo kizaazaa hutokea. EPL au LA LIGA ??????!!!!!!!!  Kila mtu huwa ana cha kwake cha kusema kuhusiana na hili lakini naomba hapa twende sawa wote.Ligi kuu maana yake ni

mashindano ya soka yanayoshirikisha mkusanyiko wa klabu bora zaidi katika nchi fulani katika idadi fulani inayopangwa na shirikisho la soka la nchi husika

.

Hivyo tukitaka kupata jibu la wazi kuhusu ligi bora ni lazima tulizingatie sana hii maana ya ligi.LA LIGA ligi kuu ya Hispania ni ligi bora sana tena zaidi ya sana kuliko duniani,lakini  ubora wa ligi hii huletwa na na timu na  wachezaji wachache sana ukilinganisha na ligi kuu ya EPL .Hivyo uwiano wa timu na ubora wa ligi kwa ujumla unakataa kwa LA LIGA na kuipendelea EPL.Kwa mfano timu bora LA LIGA ni     

 • Fc Barcelona
 • Real Madrid
 • Atletico Madrid
 • Sevilla
 • Valencia

kwa upande wa timu bora EPL timu bora ni

 • Chelsea Fc
 • Manchester United
 • Liverpool
 • Arsenal
 • Manchester city
 • Totenharm hotspurs
 • Na nyingine nyingi

kiuhalisia kila timu EPL inao ushindani wa kubadilisha matokeo na msimamo wa ligi tofauti na LA LIGA .Hivyo LA LIGA kwenye orodha hii inakuwa ya pili kwa vigezo hivyo , Najua kama tukitumia vigezo vya  wachezaji wenye majina na vipaji,ushindi wa vikombe vingi vya ligi za kimataifa,Tuzo za wanasoka bora, na ubora wa soka  LA LIGA inakuwa mfalme wa ligi duniani bila ubishi wa aina yoyote ile .Lakini ubora wa ligi ni lazima tukubaliane kuwa ushindani miongoni mwa timu za ligi husika huchangia kwa asilimia nyingi sana.

 

 

 

#1

ENGLISH PREMIUM LEAGUE

epl_0.jpg

ENGLISH PREMIUM LEAGUE

Hii ndio ligi maarufu ,yenye kutamaniwa na wachezaji wengi zaidi na yenye mashabiki zaidi kuliko ligi nyingine yoyote ile duniani.Ligi hii sio kwamba ina vitu vingi sana vinavyoipa nafasi hii adimu sana .vitu hivi vichache ni vifuatavyo

 • USHINDANI WA HALI YA JUU SANA: Tofauti na LIGA BBVA au ligi zingine ligi kuu ya Uingereza inao ushindani mkali sana kiasi kwamba kuchukua ligi hii mara mbili mfululizo hudhihirisha timu husika ni bora kiasi cha kutisha, Muda wowote timu inaweza kushuka au kupanda nafasi kwenye ligi.Sio rahisi mfungaji bora wa msimu kusikia kafikisha magoli 30 – 40 kama ilivyo kwa ligi zingine ambazo watu wanafunga kana kwamba kuna timu za watoto wanaonyonya na watu wakubwa zinazoshindana.
 • KUTOTABIRIKA :  Ligi hii haitabiriki kama zingine, sio rahisi kumjua bingwa ni nani wala wakushuka daraja ni nani, kila timu inahitaji matokeo .
 • HAMU YA WACHEZAJI JUU YA LIGI HII:   Inaaminika mchezaji akitua ligi kuu ya EPL basi atakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kufahamika haraka na kufaidi matuda ya uchezaji wake kutokana na ligi hii kuwa na  mashabiki wengi sana duniani.
 • NBA YA SOKA:   NBA ilikuwa ligi ya mpira wa kikapu Marekani mara tu baada ya timu nyingi sana bora za za mchezo huo wenye kuvutia zaidi macho kuliko mchezo mwingine kutokea zaidi Marekani . Jambo hili linataka  kujitokeza katika soka na linazidi kujijenga siku baada ya siku kutokana na  maboresho na ujenzi wa vikosi imara miongoni mwa klabu za Uingereza maana mpaka sasa kila timu inaweza kuifunga nyingine katika ligi hii.

Yapo mengi sana ya kuzungumza kuhusu ligi kuu ya EPL lakini tuishie hapo mengine yote tutazungumza kwenye ENGLISH PREMIUM LEAGUE vs LA LIGA BBVA na tutahitaji kusikia maoni yako kama mdau wa soka kumaliza huu ubishi.

LAKINI TUKUMBUSHANE KITU JAMANI:

HAPA AFRIKA MASHARIKI KUNA LIGI  ZA SOKA ZA MUDA MREFU,SIDHANI KAMA NI SAHIHI KUENDELA KUWA NYUMA KIMAENDELEO YA SOKA WAKATI VIJANA WENYE VIPAJI WAPO. HUU NI UZEMBE WA HALI YA JUU KUZIDI KUFUNGWA AU KUSHINDWA KUFUZU MASHINDANO YA KIMATAIFA.INATAKIWA TUFANYE KITU MAANA HATA TIMU NYINGINE ZINAZOFUZU NA KUCHUKUA VIKOMBE SIO KWAMBA ZINAJUA SANA KUCHEZA MPIRA KUTUSHINDA SIO KWELI ,TUSIAMINI KITU HIKI CHA KIPUUZI .INABIDI TUFANYE KITU AU SIYO ?! NI KWELI KABISA.

Wewe ni sehemu ya  www.NIJUZEPEDIA.com Toa  Maoni yako na share na wengine

Advertisements

Leave Comment / Toa Maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s