TOP 10 MIJI MIZURI ZAIDI AFRIKA MASHARIKI.

USIDANYIKE….. !  Kwamba ukanda wa Mashariki mwa Afrika eti hakuna miji mizuri sio kweli!. Miji ipo mizuri sana ambayo inafaa kabisa watu kuishi na kufurahia uzuri wa miji hii ambayo mazingira yake yamekuwa zawadi toka kwa MUNGU iliyoitoa kwa ukanda huu wa bara la Afrika.Kutokana na ushindani uliopo miongoni mwa miji ya Afrika mashariki, .Vipo vigezo vya kimataifa vilivyotumika kusema mji fulani ni mzuri ,mara nyingi vigezo hivi huzingatia muonekano wa vitu vya asili kama vile mito,maziwa,bahari,miti,milima,tambarare na kadhalika Ingawa haimanishi vitu kama mpangilio wa makazi,barabara kwamba havizingatiwi.Lakini baadhi ya vigezo vikuu ni mwonekano wa kijani(the green field), vyanzo vya maji vinavyozunguka mji(water bodies ’round city),milima,mabonde na maeneo ya tambarare katika eneo la mji,usafi na utaratibu mzuri wa kutupa taka(city clarity n’ waste managment).Fuatilia… Listi hii inakupa fursa ya kujua miji mizuri Afrika mashariki.

10.BUJUMBURA.

bujumbura-burundi
Bujumbura,Burundi

 Burundi ni nchi ndogo kwa kilomita za mraba lakini haiko nyuma unapotaja miji  mizuri ya Afrika mashariki. Bunjumbula ukiwa ndo mji mkuu wa Burundi mji huu kwa hakika ni mzuri.Uki wa na maeno mengi ya kijani ,miundombinu inayotosheleza idadi ndogo ya  watu iliyopo hufanya mji huu uonekane wenye kuvutia.Tembelea Bujumbula ujionee uzuri wa jamhuri ya Burundi.

9.NAKURU.

nakuru
Nakuru,Kenya

Hili ni jiji la tatu kwa ukubwa nchini kenya,Nakuru ni mji mzuri wenye kuzungukwa na milima ,kwa aliyefika atakwambia mwonekano mzuri Nakuru .Hatusiti kuweka jiji hili katika orodha hii ya miji mizuri ya Afrika Mashariki maana kwa hakika lina vigezo vyote vya kuwemo.Twende kenya twende Nakuru.

8.ZANZIBAR

zanzibar1
Zanzibar  Island,Tanzania

Zanzibar !! nani anakataa?!…ulizia wakazi wa Unguja na pemba uzuri wa visiwa hivi watakwambia kiasi gani wangeni wanavyovutiwa  sana na visiwa hivi.Zanzibar maarufu kama Zenji ndugu yangu  mwambao wa bahari ya hindi unaozunguka visiwa hivi kwa hakika hakuna wa kubisha hata  kidogo kwa mji huu mkongwe ni mzuri sana.Tembelea zanzibar leo urudi na marashi ya karafuu yahe na utusimulie uzuri wa zanziberii !!!…

7.KAMPALA.

kampala
Kampala,Uganda

Jiji kubwa na mji  mkuu wa nchi ya Uganda,nyumbani kwa kina Dokta Jose chamillion,Julliana,Emmanuel okwi,Michael ross na wengine wengi.Ukiwa umepakana na ziwa victoria na milima mizuri hufanya jiji hili kuonekan vizuri sana kwa vigezo hivi na vingine Kampala inaingia kwenye orodha hii bila kipingamizi chochote.

6.ARUSHA.

ar-tz
Arusha,Tanzania

Hapa ndio makuu makuu ya Afrika mashariki.”Aisee chalii wangu” Utakubali tu mwenyewe,Arusha likiwa ndio jiji la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania ,hali ya hewa ,idadi ya watu ya wastani, milima na sehemu zenye green field hufanya mji huu kuonekana vizuri.Hivyo ni lazima ukubali kuwa Arusha ni moja ya miji mizuri katika ukanda wa Afrika mashariki.

5.MOMBASA

mombasa_skyline
Mombasa,Kenya

Ushawahi fika Mombasa??!!! kama bado tafuta mtu aliyefika atakwambia mengi kuhusu mji huu ulioko pwani ya Kenya .Ukiwa karibu na bahari mji wa mombasa unavutia sana hasa wageni toka nje ya Afrika .mji huu mwonekano wake mzuri unachangiwa na eneo la pwani ya bahari ya hindi linalopakana na mji huu.Mombasa inaingia kwenye listi hii kiuhalali.Maana hata picha kwa wale ambao hawajafika zitathibitishia hilo.

4.DAR ES SALAAM

dar-es-salaam-tanzania
Dar es salaam,Tanzania

Jiji kubwa kuliko yote katika ukanda wa Afrika Mashariki likiwa na  idadi ya watu zaidi ya  milioni 4.3, zaidi ya 1000 km squares , majengo marefu zaidi Afrika Mashariki na kati ,bandari kubwa zaidi inayotengemewa na nchi jirani,Dar es salaam ni mji wa tatu kati ya miji inayokua kwa kasi kubwa  bara la Afrika na Kidunia ni  mji wa tisini na mbili(92).Licha ya idadi na ongezeko la watu kila siku serikali ya Tanzania inajitahidi kulinda na kuboresha vitu vya asili kama vile fukwe za bahari ya hindi ,kisiwa cha kigamboni kikiwa kimeunganishwa na daraja kubwa zaidi Afrika Mashariki ”Daraja la Nyerere ” .Serikali inatunza vyote hivi kwa sababu vitu hivi hufanya jiji hili lionekane zuri na lenye kupendeza.(pongezi kwa serikali ya jiji kwa kupanda miti barabarani ni jambo zuri sana la kuigwa na miji mingine)..Hivyo hakuna wa kubisha  Dar es salaam kuwa namba za juu kwenye orodha hii.

3.KIGALI.

kigali
Kigali,Rwanda

“Ibhwikongwa na majambele” Kauli inayotumika sana katika kuhamasisha maendeleo ikimanisha “kazi na maendeleo”.kabla ya kuzungumzia mji huu wa Kigali ni lazima tutoe pongeze za dhati kwa serikali ya Rwanda kwa kulifanya jiji hili kuzidi kuendelea kila kukicha. “Jiji safi kuliko yote Afrika” unategemea mji huu utakuwa mbaya ?! Haiwezekani !! Mji wa Kigali  ni mzuri sana tena sana, unazo green fields za kutosha,usafi unazingatiwa sana kiasi cha kutambulika miongoni mwa mamia ya miji ya bara la Afrika.Inafaa kuwa namba moja kigali ni mji mzuri sana na  heko kwa wanyarwanda wazidi kuboresha mji huu uzidi kupeperusha bendera ya Afrika mashariki.

2.NAIROBI

7day-nairobi
Nairobi,Kenya

“London  ya Afrika” ?!  Hakika …. hili ni jina lisilo rasmi ambalo linatolewa kutaja moja ya majiji makubwa,maarufu na mazuri barani Afrika Nairobi.Jiji kuu la nchi yenye uchumi mzuri na viwanda vya kati barani Afrika nchi ya Kenya.Nairobi uzuri wake ambao hauna haja ya kuelezewa hupeperusha bendera vyema sana ya ukanda wa Afrika mashariki.mji huu ni mzuri sana, unafaa sana  kuongoza listi hii ila kwa sababu kwa  Afrika mashariki vigezo vinavyotumika hapa vinafanya jiji hili liwe la pili katika listi hii.

1.MWANZA

rock-city-2
Mwanza,Tanzania

PUMUA KWANZA !!!! ….Yawezekena hukutegemea au hata hujawahi kufikilia kitu kama hiki.Mawazo na imani ya watu wengi inawapeleka kufikiria majiji makubwa kama Nairobi na Dar es salaam .Sikia nikwambie kitu Jiji la Paris ,Ufaransa inaaminiwa kuwa ndio mji mzuri zaidi duniani !.. ni kweli  Lakini Inakupasa uelewe kuwa wataalamu wa miji duniani huamini jambo hili mara tu  jiji la Paris linapolinganishwa na miji mingine mikubwa kama lenyewe na si vinginevyo!!!!!! KIUHARISIA jiji la Paris ni la pili kwa uzuri duniani baada ya mji ambao si maarufu sana wa Venice,Italy.Kitu hiki kinajitokeza kwenye lorodha yetu hii.JIJI LA MWANZA maarufu kama  ROCK CITY ndio mji mzuri zaidi kuliko miji mingine Afrika ya mashariki. kwa vigezo vifuatavyo.

PAMOJA na kutonadiwa(promotion) na Tanzania kama ilivyo kwa Arusha na Dar es salaam.  Mwanza ndio jiji la pili kwa ukubwa Tanzania,safi siku zote na zuri zaidi Tanzania ,Ni moja ya miji yenye green fields nyingi barani Afrika. Wenyeji wa jiji hili Wasukuma kabila kubwa kuliko mengine Tanzania ,vile vile sehemu kubwa ya ziwa la pili kwa ukubwa duniani (Victoria) linazunguka sehemu za mji huu kitu kinachofanya mji huu kuitwa Rio de janeiro ya Afrika na wageni toka nje ya bara la Afrika.

Jiji hili linahitaji maboresho na mipango mipya michache sana ili kuwa International city , Hii ni rai  kwa serikali ya jiji la Mwanza kuchukua hatua za makusudi za kuendeleza mji huu maana sio mji wa kawaida kwa jinsi ulivyo kaa ingawa watu wengi hawalioni hili. 

Mfano  Pandeni miti,ongezeni green fields nyingi iwezekwnavyo na kuongeza barabara zaidi na kuboresha mwonekano wa bandari na usafi wa mara kwa mara.kwa maana location  nzuri sana ya mji huu inaruhusu mji huu kuendelea haraka ndani ya muda mfupi sana kuliko miji mingine yote iliyoko Afrika Mashariki. Fanyieni kazi suala hili ,Mwanza litazidi kuwa jiji zuri na maarufu sana.

HIYO NDIYO ORODHA YA MIJI 10 MIZURI ZAIDI AFRIKA MASHARIKI.

UNAWEZA UKAWA HUJAKUBALIANA NAYO .

Wewe ni sehemu ya    www.NIJUZEPEDIA.COM    Toa hoja maoni yako kuhusu orodha hii.

 

Advertisements

Comments

One comment on “TOP 10 MIJI MIZURI ZAIDI AFRIKA MASHARIKI.”
  1. Hey! I know this is kind of off topic but I was wondering which blog platform are you using for
    this website? I’m getting fed up of WordPress because I’ve had problems with hackers and I’m looking at
    alternatives for another platform. I would be fantastic if you
    could point me in the direction of a good platform.

    Like

Leave Comment / Toa Maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s