Njia 10 rahisi sana za kufaulu mitihani .

YAWEZEKANA! Unasoma sana lakini matokeo yakitoka hutamani rafiki au hata wazazi wako wajue kile ulichopata AU unafanya vizuri darasani na mitihani ya kawaida lakini inapofika muda wa kufanya mitihani ya mwisho kama vile ya wilaya,mkoa na taifa unafeli mpaka unahisi unafanyiwa hila au umelogwa!.Kufeli  sio jambo zuri kwa mtu kulipata katika kitu chochote hasa ukiwa shuleni,kwa kutambua hilo haijalishi wewe ni mwanafunzi wa shule ya hadhi gani au unarudia  mtihani au wewe ni P.C  huna budi kujua njia hizi  rahisi sana za kukusaidia kufaulu mitihani yako.

1 .SOMA MITIHANI ILIYOPITA.(past papers)

Njia hii ni rahisi sana itakusaidia sana kujua namna ya kujibu maswali,kujua mitego na mbinu za watunga mitihani ambao mara nyingi hurudia maswali yaleyale kwa namna tofauti,vilevile itakusaidia kujua format au miundo ya mitihani  na hii itapelekea wewe kujua majibu ya maswali mengi sana ndani ya muda mfupi sana.Mbinu hii itakusaidia sana kufaulu mitihani.

2. JUA MADA ZOTE ZA KILA SOMO UNALOLISOMA.(Topics)

Kujua topic za kila somo unalotarajia kujibu mtihani wake kutakusaidia sana  kujua mada zipi huwa na maswali mengi,alama nyingi,mada zenye maswali rahisi na magumu.Hii inakupa mwongozo sahihi sana wa kujua wapi pa kuanzia pindi unavyojiaandaa kujibu mtihani.Ni hatari sana kuingia kwenye chumba cha mtihani ukiwa hujui maswali yapi ya kuanza kwenye mtihani husika hata kama unajua vitu vingi vya kujibu.Hivyo kujua topic ni njia rahisi sana kuelekea kufaulu mtihani wako.

3. SOMA KWA LENGO. (Target)

Kusoma sio hekali za shamba unazotakiwa kutumia muda mrefu sana ili umalize kuzilima la hasha ! kusoma ni kazi inayohusisha akili na viungo hivyo unatakiwa kuwa na lengo maalumu kila unaposoma sio kusoma ilimradi.Ni heri ulale upumzishe akili kuliko kusoma ukiwa hauelewi kitu husika unachokisoma kina faida gani kwako.Ndio maana wapo baadhi ya wanafunzi  wanaotumia muda mrefu hufeli wakati wapo watu wanaofaulu licha ya kutoingia darasani wala kusoma muda mrefu .Hii ni kwa sababu wengi wa wanafunzi wanaosoma muda mrefu husoma bila ya kujua lengo la kusoma vitu au mada fulani na kuishia kufeli.Hivyo kujua unasoma kitu fulani kwa ajiri gani kutakupa uhakika mkubwa wa kufaulu amini.

4. TUMIA MUDA MWINGI KUSOMA MASOMO UNAYOYAELEWA VIZURI. (uwekejazi)

 Usielewe vibaya ! Kutumia muda mwingi kwenye masomo unayoyaelewa vizuri haimanishi  uache kusoma masomo mengine,ila hii ina maana kwamba unatakiwa kuelewa zaidi na zaidi na kugeuza masomo yote unayoyaelewa kama uwanja wa nyumbani kiasi kwamba katika mitihani ya masomo hayo unakuwa na uhakika wa kupata zaidi ya 65% mpaka 75% .Mbinu hii ni rahisi sana na muhimu maana ufaulu hutegemea alama za masomo tofauti tofauti na sio somo moja tu.Hivyo jua zaidi kwenye masomo unayoyaelewa yatakulipa kwenye mitihani na kukupa uhakika wa kufaulu.

5.SOMA NOTES FUPI ZENYE KUBEBA MAWAZO YA MSINGI.(kupunguzia kichwa mzigo)

Badala ya kusoma maelezo mengi kama msomaji wa risala ,Notes fupi zilizo andaliwa vizuri zitakusaidia kufaulu mtihani kirahisi.Njia hii itakusaidia kutokuishiwa hamu ya kusoma unapotumia notes fupi,husaidia kuelewa haraka na kwa mujibu wa wataalamu wanadai Notes fupi husaidia sana kumtunzia mwanafunzi kumbumbu nzuri.Hivyo tumia notes fupi,mfano mzuri wa notes fupi na  nzuri ni zile zinazotolewa na application ya “thl tanzania” kwenye vifaa vya elektroniki simu,tablets n.k , vitini ,vitabu na vipeperushi mbalimbali.”Zingatia”( Hakikisha notes zako fupi zinaendana na kile ambacho mtaala unachohitaji ukisome vilevile Njia hii inaweza kutofanya  vizuri sana kwenye baadhi ya masomo mfano hisabati;fizikia na kemia na biologia,hivyo kwa masomo haya notes fupi lazima zipewe uungwaji mkono na mazoezi ya mara kwa mara  japo kwa baadhi ya watu sio lazima).

6. BUNI KANUNI ZA MAJIBU.(kuwa mbunifu)

Kubuni Kanuni ni ujanja wa aina yake asikudanganye mtu.Elewa kwanza hizi sio kanuni rasmi bali ni kanuni ambazo mtu anabuni kwa namna yake akiwa na lengo zimsaidie kutunza kumbukumbu na zimrahisishie anapojibu maswali.Yawezekana hujaelewa vizuri bado usijali ,,,Mfano mzuri wa kanuni za kubuni ni ule watoto wa shule ya msingi hufundishwa ili kukariri haraka vipimo vya urefu yaani;”Kofia Huuzwa Dukani Mwa Daudi Senti Mia” ikimanisha Kilomita, hektomita, dekamita, Mita,Desimita,Sentimita na Milimita.Hivyo ukitulia kwa kila somo lolote unaweza kubuni kanuni hizi ambazo zitakurahisishia sana kujibu maswali na kukupa uhakika wa kufaulu.

7.FANYA TATHIMINI NA FAHAMU MUDA ULIOSALIA KABLA KUFANYA MTIHANI.(uandaaji wa silaha)

Hii ni njia rahisi sana inayoweza kukufanya ufaulu mtihani tena ukiwa na uhakika.Tathimini ndio kipimo sahihi kitakacho kufanya ujue upungufu wako uko wapi na nini ufanye kulingana na muda ambao utakuwa umesalia kabla ya kufanya mtihani.Zingatia “tathimini” hii unatakiwa uifanye ukiwa peke yako au na mtu mwenye kukutakia mema kama vile rafiki yako unayesoma naye ,hapo mtagundua wapi panawasumbua na kujua wapi pakupata msaada kabla ya mtihani.Mitihani ya kujiandaa haitoshi kukwambia uko sawa ila inahitaji wewe ufanye tathimini sahihi ujue unachotakiwa kufanya kabla ya mtihani.

8. KUTANA NA WENZAKO KABLA YA SIKU AU MASAA MACHACHE KABLA YA MTIHANI.(discussion yenye mafanikio)

Hapa elewa kwanza kwenye suala la discussion kuna watu aina mbili darasani au katika kusoma;wapo watu wanopenda sana discussion lakini lazima tuelewe kuwa kuna watu wengine hawapendi kabisa kusikia kitu kama hicho sio kwamba hawapendi ushirikiano na wenzake bali hujisikia huru sana wakiwa wanasoma peke yao.Ikiwa wewe ni miongoni mwa watu wa kundu hili hapa panakuhusu .Raha ya kusoma ni kufaulu hivyo kuna hamu kubwa ya kusoma siku chache kabla ya mtihani .hivyo kama wewe hupendi discussion za kila siku discussion kabla ya kufanya mtihani zitakusaidia sana kujua mbinu za wenzio ukichanganya na zako utapata kitu.chukueni na fanyeni past papers pamoja,utapata pointi nyingi sana na haitakuwa rahisi wewe kujisahau kama unajiamini kwenye kutunza kumbukumbu nakujibu mtihani kirahisi.

9.ELEWA MAZINGIRA NA HISTORIA YA MITIHANI.(kuwa mtabiri)

Ni rahisi sana kupata O% kwenye mtihani wa midterm lakini sio rahisi kupata O% kwenye mtihani wa taifa” .Watu hawalielewi hili ,mtihani wa wilaya,mkoa au taifa siku zote unazingatia kupima wanafunzi wa kila aina,wa shule zenye waalimu,wa shule zenye uhaba wa waalimu na hata wale watihaniwa wa kujitegemea.Hivyo maswali hutolewa  kwa kuzingatia mtaala wa taifa na sio wa shule wala kituo cha elimu.Kwa kujua hili sio rahisi kufeli ina maana lazima utajua tu maswali ya muhimu ambayo ni lazima yatoke kwenye mtihani ,maana siku zote mtaala wa elimu ni uleule na hata mabadiliko yakitokea serikali hutangaza.Hivyo kwa nini usifaulu mtihani wakati unaelewa mada na  maswali yake?!.

10.TULIA,KUWA NA AMANI FANYA MTIHANI.(usiwaze kuhusu matokeo,likizo au kumaliza shule)

TULIA !!! Unawaza kuhusu kumaliza mtihani sio?! Tulia ratiba ikiisha utarudi mtaani, hivyo usiruhusu kufikiria mambo mengine badala ya mtihani muda wa mtihani, japo hutokea kwa baadhi ya watu .mfano wale wanaofikwa na matatizo mbalimbali kabla au kipindi cha mtihani sio rahisi kutofikiria matatizo hayo,lakini usijali….Jitahidi kuwa Strong na muombe MUNGU.Lakini kama hauna tatizo lolote muda wa mtihani sio muda wa kufikiria kuhusu likizo au nini utafanya baada ya mtihani ,muda wa mtihani ni muda wa kuandaa kile kitakacho onekana baada ya mtihani na si vinginevyo.Ingawa wapo watu wengi sana wanaotumia muda huu vibaya kwa kuwaza nyumbani,na mambo mengine yasiyo sahihi kwa muda huo.Tasisi za Elimu au shule si miaka ya kukufanye ukue bali ni mahali ambapo wazazi,walezi au hata taifa linategemea utoke na ujuzi utakotufaa watu wote hivyo tafadhali usituangushe.

ZINGATIA:

Njia hizi ni za uhakika kutokana na mafanikio watu wengi waliotumia njia hizi kufaulu.Kila mtu ni shahidi mazingira ya shule nyingi si rafiki sana kwenye kufaulu kutokana na mapungufu mbalimbali ambayo serikali haiwezi kuyatatua peke yake.hivyo hakuna wa kumlaumu kwenye matokeo mabovu yanayotokea maana serikali ni Mimi,wewe na yule tushirikiane,watu wafaulu nchi iwe na wasomi wenye kuelewa mambo .LAKINI tusiishie kufaulu bila ya kuwa wabunifu maana hakuna tutakacho kuwa tunakifanya.SOMA, FAULU, KUWA, MBUNIFU TUPATE MAENDELEO YA KWELI.

SHARE NA WENZIO

Advertisements

Leave Comment / Toa Maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s